WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kujiuzulu wadhifa huo ifikapo tarehe 7 Juni 2019, kufuatia mkakati wake wa kuliondoa taifa hilo kwenye Umoja wa Ulaya (EU) kukwama. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
May ametangaza hayo leo tarehe 24 Mei 2019 akiwa mjini Downing Street, Uingereza.
Amesema, anajutia kitendo cha kukwama kwa mpango wake huo unaofahamika kama Brexit na kwamba, kwa maslahi ya taifa hilo, amejiuzulu ili lipate waziri mkuu mpya akiamini kwamba, ndiye atakayekuwa suluhu.
Kufuatia hatua hiyo, May ataendelea kushikilia wadhifa huo hadi pale mchakato wa upatikanaji wa waziri mkuu mpya utakapokamilika kwa kiongozi mpya kuchaguliwa.
Aidha, May amejiuzulu wadhifa wa uongozi wa chama cha Conservative na kwamba taachia ngazi rasmi tarehe 7 Juni 2019.
Leave a comment