Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Manyanya avutiwa ujenzi wa madarasa
Habari Mchanganyiko

Waziri Manyanya avutiwa ujenzi wa madarasa

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya
Spread the love

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amewataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa wazalendo kwa nchi yao huku akiwaasa kutumiwa katika mambo yote yenye vurugu, anaandika Mwandishi Wetu.

Naibu waziri mhandisi Manyanya ametoa rai hiyo  wilayani Korogwe mkoani Tanga katika ziara yake aliyokuwa akiieleza kuwa ya kujifunza suala la fedha kidogo kazi ikiwa bora.

Katika ziara yake hiyo Naibu waziri alitembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari huku akipongeza jitihada za ofisi ya mkuu wa wilaya ya Korogwe, Robart Gabriel katika kusimamia kazi hiyo yenye ubora.

Aidha, alipokuwa kwenye maeneo ambayo ujenzi huo umefanyika ambako alikutana na wanafunzi alitumia fursa hiyo kuwaasa kuzingatia masomo badala ya kutumika kwenye vurugu huku akiwasisitiza uzalendo kwa nchi.

Akizungumzia zaidi alichokiona kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa Naibu waziri Manyanya alisema ameridhishwa na kazi iliyofanyika kwa ushirikiano wa DC Korogwe na wananchi wake.

Amesema Mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe ni jembe la ukweli linalopaswa kuwa mfano wa kuigwa ambapo hakuna haja ya kufanyiwa ukaguzi kazi zake zinajieleza huku akimhimiza kuendelea kuchapa kazi kwa bidii.

“DC ni jambe…jembe la ukweli hakuna haja ya DC kufanyiwa ukaguzi kazi zake zinajieleza atapimwa kwa jitihada zake za utendaji,” amesema.

Amesema kilichompeleka Korogwe ni kutaka kujifunza utaratibu ambao umekuwa ukifanyika kwenye ujenzi ambapo fedha ndogo zikekuwa zikitumika kwenye utekelezaji huku kazi ikiwa yenye viwango vya ubora.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Korogwe mhandisi Robert Gabriel amemweleza Naibu waziri huyo kuwa kabla ya fedha za serikali kuanza kutumika kwenye eneo lake lazima zipitie ofisini kwake ili kuweka udhibiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!