Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Majaliwa: Serikali inaendelea kupambana na mafisadi 
Habari Mchanganyiko

Waziri Majaliwa: Serikali inaendelea kupambana na mafisadi 

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kupambana na wala rushwa pamoja na mafisadi wote ambao walikuwa wanakula fedha za miradi ya maendeleo na kusababisha kushindwa kutekelezeka kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya maji. Anaripoti Moses Mseti, Misungwi … (endelea).

Amesema Serikali itahakikisha fedha ambazo zilikuwa zinapigwa na mafisadi, zinarudi kwa wananchi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo kwa sasa inaendelea kujengwa nchini.

Pia amesema serikalii ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli imejikita katika kupambana na mafisadi ambao kazi yao walikuwa wanakula fedha za miradi ili kuhakikisha fedha hizo zinafanya maendeleo yaliyokusudiwa.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji kata ya Nyahiti wilayani Misungwi, unaojengwa kwa gharama ya Sh. 12.85 bilioni kwa ufadhili wa benki ya uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFP) na serikali ya Tanzania.

Waziri Majaliwa amesema mipango yao ni kutaka kuhakikisha mwananchi wa kawaida ambae alikuwa anaona serikali haina msaada kwake, sasa aanze kuona msaada wa serikali yake kwa kutekeleza miradi ya maendeleo nchi nzima.

Amesema miradi yote ya maji ikiwemo huo wa Nyahiti serikali imekusudia kuikamilisha kwa wakati na kwamba katika mradi huo wa Nyahiti ambao mkandarasi anadai Sh. 600 milioni serikali kwa kuanza itamlipa milioni 400 na nyingine atalipwa pindi akikamilisha mradi.

Majaliwa amesema mipango ya serikali ni kutaka kukamilisha kwa kipindi kifupi miradi yote ya maji nchini ambayo mingine serikali imetoa fedha za ujenzi hatua ambayo ili kwennda kuwanufaisha wananchi.

“Huu mradi tumefikia hatua nzuri sana na mradi huu unapeleka maji katika mjini wetu wa misungwi na nyie wote mnafahamu kwamba Mwanza sasa inafurika mji unakuja unakuja misungwi lazima tujiandae kuiweka vizuri Misungwi ili kupokea mafuriko ya watu wanaokuja.

“Mpango wa Rais John Magufuli ni kutaka kuona kila kijiji kuna kisima cha maji na kwenye maji tuna kampeni maalumu inaitwa kampeni ya kumtua ndoa mama kichwani tunapokuwa na maji kwenye kila kijiji ule umbari na ile kuhangaika hakupo tena hata yule ambae yupo jirani na kisima atabeba ndoo mkononi hataweka kichwani tena,” amesema Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema pamoja na serikali kuwa na mpango wa kufikisha maji kila kijiji lakini, pia katika wilaya ya Misungwi ambao ilikuwa ina tatizo la maji ina miradi mikubwa minne ambayo fedha zake zimetolewa tayari.

“Kuna mradi huu ambao tumeleta zaidi ya Sh. 700 milioni kwenye kijiji cha Igenge, mradi mwingine wa Sh. 2.4 bilioni katika kata ya mbalika mpaka Ngaya pia tuna mradi wa Sh. 1.2 bilioni ambao unatoa maji matale kwenda Manawa mpaka misasi kote huko tunapeleka maji,” amesema Waziri Majaliwa.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Professa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa miradi ya maji ni utekelezaji wa sera ya maji inayoelekeza kuwapatia wananchi maji safi na salama kwa asilimia 90 kwenye miji ya wilaya na asilimia 95 miji ya mikoa pamoja na 85 kwa wananchi wa vijijini ifikapo mwaka 2020.

Professa Mbarawa amesema mji wa misungwi pamoja na kuwa kandokando mwa ziwa Victoria lakini umekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa muda mrefu.

Amesema uzalishaji wa sasa wa maji katika wilaya ya Misungwi ni lita laki sita na hamsini elfu kwa siku sawa na asilimia 17 tu ya mahitaji ya wakazi wa mji huo na kwamba kwa kulitambua hilo serikali iliamua kujenga mradi huo mkubwa.

“Mradi huo una uwezo wa kuzalisha maji lita Sh. 4.5 milioni kwa siku ambazo zitatosheleza mahitaji kwa wakazi wote  wa mji wa Misungwi ambapo kwa sasa wanahitaji lita Sh. 3.9 milioni kwa siku, mradi huu pia umewekewa nafasi ya kuongeza uzalishaji mpaka kufikia lita Sh. 6 milioni kwa siku,” amesema Mbarawa.

Serikali pia inatekeleza mradi mkubwa wa maji unaotoa maji ziwa Victoria kwenda Nzega Igunga na Tabora ambao unagharimu kiasi cha Sh. 605 bilioni na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!