Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri azuia wananchi kumpongeza Rais Magufuli
Habari za Siasa

Waziri azuia wananchi kumpongeza Rais Magufuli

Spread the love

LUHAGA Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  amepiga marufuku makongamano ya wafugaji ya kumpongeza Rais John Magufuli,  kwa muda mpaka pale kazi waliyopewa kama Tume itakapokamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na Wananchi wa Kisesa mkoani Mwanza amesema kuwa huu siyo muda wa kuandamana na badala yake watumie muda  huo kuisaidia tume iliyondwa na Rais kwa ajili ya kusuluhisha migogoro ya ardhi kwenye jamii ya wafugaji na wakulima.

Rais Magufuli ameunda tume maalumu ya uchunguzi ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwenye jamii za wafugaji na wakulima.

Baadhi ya mawaziri kwenye tume hiyo ni pamoja Mpina, William Lukuvi, Waziri wa Ardhi  na Dk. Hussein Mwinyi,mn Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mpina amesema tume nyingi zilizoundwa miaka ya nyuma kushughulikia migogoro hiyo zilichakachuliwa hata kabla ya kukabidhi matokeo ya mambo waliyobaini kwa kuwa kwenye migogoro hiyo wako baadhi ya viongozi wa Serikali wako nyuma wana manufaa binafsi wanayopata ndio maana mapendekezo yaliyotolewa ya kutatua migogoro hiyo hayajawahi kutekelezwa hadi leo.

Amesema baadhi ya watendaji wa serikali walilazimika hata kutoa rushwa ili kubadilisha maamuzi ya tume zilizokuwa zinaundwa kushughulikia migogoro hiyo kwa sababu wananufaika na migogoro hiyo.

“John Pombe Magufuli akasema hapana nitaunda tume ambayo haitapokea rushwa timu ya Lukuvi mnaiona ina sura ya kupokea rushwa?

“Vichwa vya kina Mpina unaweza ukawapa nini wakakubali, akasema wananchi wangu watahangaika mpaka lini, watauana mpaka lini mifugo mingi imedhulumiwa kwa kivuli cha uhifadhi, Rais akasema nitaunda tume ndio hii sasa ya mawaziri,” alisema Mpina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!