Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri atetea mbinu ya trafiki kujificha
Habari za Siasa

Waziri atetea mbinu ya trafiki kujificha

Askari wa barabarani akijificha na tochi ya kudhibiti mwendo
Spread the love

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema, mbinu ya askari wa usalama barabarani (Trafiki) kujificha kwa ajili ya kubaini madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani, imechangia kupunguza ajali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mhandisi Masauni amesema hayo leo tarehe 6 Mei 2019 bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Mariamu Sabaha aliyehoji hatua zilizochukuliwa na serikali kwa trafiki wanaotumia njia hiyo, akidai kwamba imesababisha baadhi ya ajali.

Akijibu swali la Mariamu, Mhandisi Masauni amesema, askari wa usalama barabarani wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria za Usalama Barabarani.

Na kwamba, ili kutekeleza majukumu yao, huanzisha mbinu mbalimbali ambazo hazivunji sheria katika kudhibiti madereva wanaokiuka sheria na kusababisha ajali.

Mhandisi Masauni amesema, tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, kulikuwepo na ajali za mara kwa mara ambazo nyingi zilizosabaishwa uzembe wa baadhi ya madereva wasiofuata sheria za barabarani. Na kwamba, askari wa usalama barabarani walibuni njia hiyo ya kujificha ili kubaini madereva wanaokiuka sheria hizo.

Amesema, tangu askari wa usalama barabarani watumie mbinu hiyo, ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 43.

“Jeshi la Polisi nchini chini ya Sheria ya Usalama Barabarani inamtaka askari kusimamia usalama barabarani, wanatumia mbinu mbalimbali kwa mujibu wa sheria, itakumbukwa serikali ilipoingia madarakani kulikuwa na ajali nyingi hasa inayohusisha daladala za abiria,” amesema Mhandisi Masauni na kuongeza;

“Mkakati wa kupunguza ajali za barabarani ulisaidia kupunguza ajali zaidi ya asilimia 40.Mkakati huo ulihusisha mbinu mbalimbali zenye lengo la kulazimisha dereva kufuata sheria, serikali haina ushahidi wa ajali zilizosababishwa na trafiki kujificha.”

Amesema, Trafiki wana nia njema wanapotumia njia ya kujificha kubaini madereva wasiowaaminifu, na wala hawana dhamira ya kubughudhi wananchi, na kwamba kama njia hiyo ina usumbufu serikali itaangalia namna ya kuondoa.

“Kama nilivyojibu swali langu la msingi kwamba, tumepunguza ajali kwa asilimia 43 zinazosababishwa na daladala za abiria, upungufu huo ulisababishwa na mbinu na weledi wa askari wetu katika kubaini mbinu za madereva wasio waaminifu kukeuka sheria.

“Malengo yake ni njema na kama kutakuwa na upungufu kwa askari hao tutachukua kama changamoto, lengo sio kubughudhi wananchi, isipokuwa ni kukabiliana na madereva wavunjifu wa sheria.”

Wakati huo huo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Marry Mwanjelwa amesema takribani watumishi 500 waliondolewa kazini kwa kosa la kudanganaya taarifa za kitalaaluma wamerejeshwa kazini baada ya kuomba msamaha.

https://www.youtube.com/watch?v=mioUrcbYAok

Dk. Mwanjelwa amewataka watumishi waliondolewa kazini kwa sababu hiyo, kuwasilisha vyeti vyao vya taaluma wizarani kwake, ili vipitiwe na warejeshwe kazini.

“Kama walidanganya kutoa taarifa hawataruhusiwa kuwa mtumishi wa umma, serikali ilitoa msamaha hadi Desemba 2017 wale waliokuwa wamejiendeleza walete taarifa zao utumishi. watumishi zaidi ya 500 wamesharejeshwa, na wale ambao walijiendeleza baada ya muda huo walete vyeti vyao tuweze kuhakiki warejeshwe kazini,”amesema Dk. Mwanjelwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!