Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri ‘aikoromea’ Kampuni ya KEC
Habari za Siasa

Waziri ‘aikoromea’ Kampuni ya KEC

Dk. Medard Kalemani
Spread the love

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya KEC International Limited,  anayetekeleza mradi mkubwa wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Zuzu jijini Dodoma kukamilisha kazi hiyo ifikapo tarehe 28 Februari 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pia ametangaza kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watendaji wanaosimamia mradi huo endapo hautakamilika kwa muda huo kutokana na uzembe. Kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 640.  

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Februari 2020,  wakati alipofanya ziara kwa mara ya tatu katika kituo hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Dk. Kalemani amefafanua, mradi huo ni muhimu kwa Watanzania hasa wakazi wa Dodoma, kwa kuwa baada ya kukamilika kituo hicho, kitakuwa na uwezo wa Megawati zaidi ya 600, na kuwa kituo cha kwanza Tanzania kinachozalisha umeme kwa wingi.

Amesema, serikali haiwezi kuvumilia uzembe na kwamba, wanaweka vibarua wachache hivyo kusababisha kazi kuzorota.

“Nawataka muongeze vibarua, hili agizo nalitoa mara ya pili leo, anataka (mkandarasi) niwaongezee mpaka mwezi Machi, hilo haliwezekani.

“Mradi ulipaswa kukamilika Februari na ikifika Februari 28, muwe mmekamilisha, la sivyo nitaondoka na watu hapa, lazima tutachukua hatua, siwezi kukubali watanzania walale gizani,” amesema.

Na kwamba, hivi sasa kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha megawati 48, matumizi halisi kwa mkoa kutokana na ongezeko la watu ni 40, ambapo wanabaki na akiba ya megawati nane ambayo ni ndogo.

“Sasa Dodoma italipita hata Jiji la Dar es Salaam ambalo linaongoza kwa sasa kwa kuwa na megawati takribani 587, napenda niishukuru sana serikali kupitia kwa Mheshimiwa Rais kwa kutupatia Dola za Marekani milioni 52 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!