Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri aagiza kupatikana hati za viwanja vya TAA
Habari Mchanganyiko

Waziri aagiza kupatikana hati za viwanja vya TAA

Mhandisi Atashasta Nditiye
Spread the love

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ametoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuanzisha kitengo cha utafiti ili kupata hati za viwanja vya TAA ili kuondoa migogoro baina yao na wananchi. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Nditiye amesema kuwa Serikali imechoka kulipa fidia kila mwaka kwenye viwanja ambavyo havina hati hivyo amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TAA aandae kitengo maalum kisichozidi watu kumi kwa ajili ya kuhakikisha kila kituo cha ndege nchini kinachomilikiwa na TAA kinakuwa na hati.

“Mara ya mwisho nilivyokuja mwezi wa pili kulikuwa na viwanja nane vyenye hati nchi nzima, ni aibu sasahivi ndio unaniambia viko 11 bado ni aibu, najua Songwe kuna mgogoro, Mwanza kuna mgogoro, Mtwara ndio kidogo kuna nafuu nafuu lakini nadhani kila mkoa kuna mgogoro,” amesema.

Nditiye amesema kuna mgogoro kwa wakazi wa Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ambao walikuwa na malalamiko ya malipo ya fidia kutoka kwenye kampuni ya Re/max Tanzania iliyoingia ubia na Manispaa ya Temeke.

“Baadhi ya viwanja haviwezi kujengeka kwa mwananchi wa kawaida sijajua ni kwanini Tanzania Re/max mliamua kupima maeneo ambayo mwananchi wa kawaida hawezi kujenga, ninadhani wananchi watavikubali viwanja 537 ambavyo serikali ilitoa pesa kwenu muweze kuwagawia wananchi, kama kama hawatavikubali miwe tayari kwa haraka kuwapatia viwanja mbadala,” amesema.

Amesema kuwa ifikapo siku ya Jumanne kuhakiki wanafika kuvitembelea viwanja hivyo 537 na baada ya hapo atapita siku ya Alhamis kwa ajili ya kuwaita wananchi na kuwagawia viwanja vyao.

“Ipo changamoto kwa wananchi waliopewa viwanja kwa awamu ya kwanza wananchi wa Kipawa na Kigilagila ninazo taarifa kwamba wafanyakazi wasio waaminifu wa TAA walijigawia viwanja hivyo, mfuatilie yule ambaye ana kiwanja lakini sio muadhirika wa maeneo hayo mnampokonya na mnamfungulia mashitaka ya kusema uongo, watu wote walioathirika pale wanajulikana na picha zao zipo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!