WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amezitaka hosptali za wilaya kuanzisha dirisha maalum la wazee ili kuwapunguzia changamoto pindi wanapohitaji huduma za matibabu, anaandika Hamisi Mguta.
Waziri Mwalimu ameyasema hayo jana katika Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa matibabu ya bure kwa wazee ambayo itatolewa kwa wazee waishio ndani ya eneo hilo ambao wanafikia 7,299.
Wazee wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa malipo kwa huduma za afya katika hospitali za serikali.
“Kuwa na vitambulisho ni jambo moja na kupata huduma ni jambo la pili, vitambulisho hivi viwe sehemu ya wazee kupata huduma bora za afya, siyo mzee anaenda na kitambulisho anaambiwa dawa hakuna kanunue, hakutakuwa na ulazima kupatiwa vitambulisho,” amesema
Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, amaesema Sh. 1.805 kwa mwaka zitatumika kwa mwaka mmoja ili kuwahudumia wazee hao kwa vipimo, matibabu na vifaa tiba bure.
Leave a comment