Wazee Chadema wataka mwakilishi bungeni

IKIWA leo tarehe 1 Oktoba 2018, ni kilele cha siku ya maazimisho ya Wazee Duniani, wazee wameitumia siku hii kuiomba serikali kuhakikisha kundi hilo linapata wawakilishi bungeni na katika mabaraza ya madiwani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo na Baraza la Wazee la Chadema, ambapo limesema wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo serikali hushindwa kuzitambua kutokana na kukosekana kwa watu maalum wa kuwasemea kundi hilo katika vyombo vya maamuzi ikiwemo bunge na baraza la madiwani.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema, Roderick Lutembeka ameshauri kuwepo viti maalumu bungeni kwa ajili ya wazee ili kundi hilo lipate watu maalum wa kueleza changamoto zao bungeni.

Vile vile, Lutembeka ameitaka serikali kuanzisha chombo maalum kwa ajili ya kushughulikia changamoto za wazee hususan kuwepo wizara maalum itakayoshughulikia masuala ya wazee.

IKIWA leo tarehe 1 Oktoba 2018, ni kilele cha siku ya maazimisho ya Wazee Duniani, wazee wameitumia siku hii kuiomba serikali kuhakikisha kundi hilo linapata wawakilishi bungeni na katika mabaraza ya madiwani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea). Ombi hilo limetolewa leo na Baraza la Wazee la Chadema, ambapo limesema wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo serikali hushindwa kuzitambua kutokana na kukosekana kwa watu maalum wa kuwasemea kundi hilo katika vyombo vya maamuzi ikiwemo bunge na baraza la madiwani. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema, Roderick Lutembeka ameshauri kuwepo viti maalumu bungeni kwa ajili…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram