TAASISI ya Maendeleo ya Binadamu ya Chuo Kikuu cha Aga Khani, imewaomba wadau mbalimbali kufunya uwekezaji wa muda mrefu kwa watoto wa chini ya miaka miatno, anaandika Angel Willium.
Hatua hiyo imeelezwa kwamba inasaidia kujenga nafasi salama kwa ajili ya watoto.
Mkurugenzi wa Foundation IHD, Kofi Marfo, amesema hayo leo wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa wadau wa masuala ya watoto unaoendelea jijini Dar es Salaam.
“Tuna jukumu la pamoja la kujenga nafasi salama kwa ajili ya watoto ili kuwapa watoto elimu, lishe bora na afya.,’’ amesema
Aidha, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khani, Joel Lugalla amesema, jamii ikizingatia suala la elimu itasaidia watoto chini ya miaka mitano kupata malezi bora.
Lugalla amesema IHD inafanya kazi ya kuzalisha ujuzi mpya kupitia tafiti mbalimbali.
Mada zilizo jadiliwa ni pamoja na umuhimu wa utunzaji wa watoto chini ya miaka mitano.
Leave a comment