Wawa, Miquison warejea kikosini, Kuwavaa Namungo Jumapili

Spread the love

WACHEZAJI wa klabu ya Simba, Pascal Wawa na Luis Miquison wamerejea leo kikosini kwa kuingia kambini baada ya kuwasili leo nchini kutoka kwenye nchi zao walipokuwa wameenda kimapumziko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wachechaji hao ambao wamerudi nchini leo mchana na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Jijini Arusha ambapo Simba itakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Wachezaji hao waliondoka nchini mara baada ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20 kumalizika na wote kwa nyakati tofauti walienda kufunga ndoa.

Miquison alifunga ndoa yake na mwenza wake tarehe 22 Agosti, 2020 kama taarifa kutoka kwenye uongozi wa klabu hiyo zilivyoeleza.

Taarifa za kurejea kwao zimetolewa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

WACHEZAJI wa klabu ya Simba, Pascal Wawa na Luis Miquison wamerejea leo kikosini kwa kuingia kambini baada ya kuwasili leo nchini kutoka kwenye nchi zao walipokuwa wameenda kimapumziko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam ... (endelea). Wachechaji hao ambao wamerudi nchini leo mchana na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Jijini Arusha ambapo Simba itakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Wachezaji hao waliondoka nchini mara baada ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20 kumalizika na wote kwa nyakati tofauti walienda kufunga ndoa. Miquison alifunga ndoa yake na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!