WAVUVI takribani 16 kutoka Tanzania wamekamatwa nchini Kenya Jumapili tarehe 18 Novemba 2018, kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kutumia vifaa haram vya uvuvi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Watanzania hao wanadaiwa kukamatwa katika ufukwe wa Bamgot karibu na Ziwa Victoria ulioko Kaunti ya Migori, na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha Macalder huku boti zao zikizuiliwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Migori, Joseph Nthenge amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi juu ya madai yao kukamilika, ambapo kwa sasa maafisa wa polisi wanawahoji.
Sekeseke la wavuvi katika nchi zinazozunguka na kutumia ziwa Victoria, limepamba moto baada ya siku za hivi karibuni, wavuvi wa Kenya wanaotumia ziwa hilo, kudaiwa kukamatwa na vyombo vya dola vya nchi za Tanzania na Uganda.
Leave a comment