Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Wavamizi mwendokasi, hakuna faini ni mahakamani’
Habari Mchanganyiko

‘Wavamizi mwendokasi, hakuna faini ni mahakamani’

Spread the love
MADEREVA wa vyombo vya moto vinaovamia barabara ya mabasi ya mwendakasi, hawatotozwa faini badala yake watapelekwa mahakamani. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).

Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema hivyo kwa kuwa, madereva wavamizi wa barabara hizo imeongezeka maradufu.

SACP Lazaro Mambosasa,  kamanda wa polisi wa kanda huyo leo tatehe 1 Oktoba 2019 ametoa taarifa hiyo baada ya kujiridhisha kwenye oparesheni maalum ya kukamata magari iliyoanza tarehe 19 Septemba 2019.

Mambosasa amesema, kuna baadhi ya magari ya umma na binafsi yanatumia barabara maalumu za mabasi yaendayo kasi, wakidhani watalipa faini.

“Mabasi haya yametengewa njia kwa matumizi maalum, ninajua watu wana salio la kutosha. Anaandaa pesa halafu anakwenda kuingia kwenye mwendokasi akitegemea atalipa faini 30,000.

“Katika mwendokasi sitakubali kutoza faini, hatutatoza faini hatupo kwa ajili ya kutafuta fedha, tunachotaka ni kuweka nidhamu ya matumizi sahihi ya barabara hiyo,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa madereva wote hasa kuhakikisha wanatii sheria na taratibu za barabara hiyo ili kuepukana na kadhia hiyo.

Katika oparesheni hiyo, jumla ya magari 50 yamekamatwa huku 19 yakiwa mali ya serikali huku 31 yakiwa ya watu binafsi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!