Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Francis Michael

Watumishi waliogombea ubunge wakashindwa warejeshwa kazini, waonywa

Spread the love

WATUMISHI wote wa umma waliokuwa wametangaza nia kugombea ubunge na kushindwa katika kura za maoni, wametakiwa kurudi kazini kuanzia kesho Jumanne tarehe 1 Septemba 2020 kuendelea na utumishi wao wa nafasi walizokuwa wamezikaimisha. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 na Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Francis Michael wakati akitoa elimu kwa watumishi wa wizara ya maji juu ya makatazo yanayopaswa kuzingatiwa na watumishi wa umma katika  kipindi cha uchaguzi.

Michael alisema tayari waraka wa kuwarejesha kazini umeshatoka na wataanza kulipwa mshahara wa Septemba.

Watumishi hao wameonywa kutojihusisha na vurugu zozote zinazoweza kutokea kipindi cha uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 na atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

Michael alisema, kumekuwa na maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa watumishi wa umma waliokwenda kutia nia hawatakiwi kurudi kazini na kurudi kwenye nafasi zao.

“Kauli hizo si za kweli kwani kwa mujibu wa Katiba walikuwa na haki ya kugombea kwa utaratibu wa kuchukua likizo ya bila malipo na sasa muda wao wa likizo umekwisha wanapaswa kurejea kazini,” alisema Michael.

Mkutano Mkuu wa CCM

“Mtumishi wa umma, anapaswa kupiga kura, kujiunga na chama chochote cha siasa kasoro makundi machache ambayo sheria imeyakataza, hivyo muda wa kugombea utakapomalizika likizo za bila malipo walizoomba zinamalizika na wanapaswa kurejea kazini na kuanza kulipwa mshahara wao waliorejea kama kawaida,” alisema.

Michael alisema,  yapo makundi ya watumishi wa umma ambayo sheria inawakataza kujiunga, kujihusha na chama chochote cha siasa wala kugombea lakini wana haki ya kupiga kura na kumchagua mgombea wanayeona anafaa.

Naibu katibu mkuu huyo, aliyataja makundi ya watumishi wa umma wasio ruhusiwa kujihusisha na siasa ni pamoja na majeshi yote, Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ofisi ya mwanasheria mkuu, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, ofisi ya Bunge, majaji na mahakimu, wawakili wa serikali, idara ya usalama wa taifa na uhamiaji.

“Yapo makatazo ambayo yamewekwa kwa watumishi wa umma ya kutojihusisha nayo katika kipindi cha uchaguzi ni pamoja na kutojihusisha na siasa mahala pa kazi, kutovaa sare za chama chochote cha siasa maeneo ya kazi, kutotoa huduma kwa upendeleo kutokana na kuwa muumini wa chama fulani cha siasa,” alisema.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema

“Makatazo mengine ni, kutotoa siri ama nyaraka zozote za serikali kwa manufaa ya chama cha siasa kwa kutumia madaraka yao na uanachama wa chama husika, kuepuka kutumia ushawishi kwa manufaa binafsi kwa sera zisizo za serikali,” alisema.

Kuhusu wasaidizi wa viongozi wakiwemo mawaziri, Michael alisema, hawaruhusiwi kushiriki na kufanya kazi zao endapo mkuu wake wa kazi atakuwa amegombea na endapo atataka kushiriki itabidi achukue likizo ya bila malipo na akitaka kurejea ataandika barua ya kurejea.

“Kushiriki kwa wasaidizi hao au magari ya serikali kunaweza kumsababishia mgombea kuvuliwa ubunge endapo itabainika ushindi wake umechangiwa au kutokana na jitihada hizo na gari la serikali kutumika kwenye kampeni,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Mwanasheia Mkuu wa Serikali, Evaristo Lungopa, alisema  Ibara ya 18, 20 na 21 ya Katiba, inazungumzia haki ya kutoa maoni, uhuru wa kutoa maoni, haki ya kujiunga na chama cha siasa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mtumishi wa umma ukiacha makundi ambayo yanakatazwa kujihusisha na siasa.

Pia, alisema, watumishi wa umma wanakatazwa kutamka au kutoa matamko yanayodhalilisha serikali, kutumia magari au madereva wa serikali kufanyia kampeni, katiba inaelekeza mtumishi yeyote atakayekuwa amekiuka kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

WATUMISHI wote wa umma waliokuwa wametangaza nia kugombea ubunge na kushindwa katika kura za maoni, wametakiwa kurudi kazini kuanzia kesho Jumanne tarehe 1 Septemba 2020 kuendelea na utumishi wao wa nafasi walizokuwa wamezikaimisha. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). Kauli hiyo imetolewa jana Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 na Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Francis Michael wakati akitoa elimu kwa watumishi wa wizara ya maji juu ya makatazo yanayopaswa kuzingatiwa na watumishi wa umma katika  kipindi cha uchaguzi. Michael alisema tayari waraka wa kuwarejesha kazini umeshatoka na wataanza kulipwa mshahara wa Septemba. Watumishi hao wameonywa kutojihusisha na vurugu zozote zinazoweza kutokea…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!