Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Watumishi TAA walia njaa, Waziri awapotezea
Habari za SiasaTangulizi

Watumishi TAA walia njaa, Waziri awapotezea

Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam
Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayogela, amesema wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wanakabiliwa na njaa (ukata) licha ya kuwa wanaonekana kupendeza wanapokuwa wamevaa suti wakiwa katika vikao au mikutano. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mayogela amesema kuwa kinachosababisha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kukabiliwa na njaa kali ni kutokana na kuwepo kwa changamoto ya watumishi wake kuwa na mishahara midogo pamoja na malupulupu yasiyotosha.

Mkurugenzi huyo alitoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini.

“Muheshimiwa Waziri hapa unapotuona sisi leo hii tumependeza lakini ni kwa sababu tumevaa suti lakini ukitukuta katika maeneo yetu ya kazi utatuonea huruma kiukweli tuna njaa kubwa sana na sura zetu zinakuwa zimekunjamana,” alisema Mayogela.

Aliongeza kuwa pamoja na changamoto hiyo lakini wao kama mamlaka wanafanya kazi kwa kujituma ili kufikia malengo ya serikali ya kufikia uchumi wa kati.

“Hivi sasa tunakusanya kiasi cha Sh. 70 bilioni kutoka Sh. 3 bilioni ambayo ilikuwa inakusanywa mwaka 1999 hivyo basi ipo kila sababu ya serikali kutuangalia kwa jicho la huruma kutuongezea mishara pamoja na maslahi mengine,” alisema Mayogela.

Pamoja na Mkurugenzi huyo kueleza kuwa watumishi wanakabiliwa na njaa, Serikali  imesisitiza kuwa kamwe  haitaongeza mishahara wala malupulupu kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini (TAA) hadi hapo itakapoona ukusanyaji wa mapato umepanda tofauti na ilivyo sasa.

Mbali na hilo imeeleza kuwa moja kati ya changamoto ambazo zinachangia Mamlaka hiyo kufanya vibaya kwa sasa ni kutokana na kukosa wataalam wenye weledi juu ya masuala ya mambo yahusuyo viwanja vya ndege.

Alisema serikali kwa wakati huu haiwezi kuongeza mishahara wala malupulupu kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo kutoka na kukusanya kiasi kidogo cha mapato.

Mhandisi, Kamwele alisema kuwa serikali itakuwa tayari kuongeza mishahara kwa wafanyakazi hao kama wataongeza ukusanyaji wa mapato katika kiwango cha juu tofauti na ilivyo sasa.

“Kwa sasa kuongeza mishara itakuwa ngumu sana, ongezeni kwanza ukusanyaji wa mapato halafu ndipo tutaona nini cha kufanya kama mtakusanya zaidi hakuna atakayekataa kuwaongeza mishahara kwani fedha ni zenu,” alisema Mhandisi Kamwelwe.

Aidha aliitaka Mamlaka hiyo kubadilika katika utendaji wake kazi ili kuweza kuendana na mikakati ya serikali kuelekea uchumi wa kati.

“Hivi sasa nataka kuwaongezea jukumu la kuanza kuendesha hivi viwanja vya ndege badala ya kuwatumia watu wengine lakini pia hata kuuza mafuta ya ndege mtafanya nyie lakini kama hamtabadilika hatuta toka hapa tulipo kwani nafahamu huku nakotaka mwende kusimamia kuna mapato mengi zaidi,” alisema.

Akizungumzia juu ya watumishi wenye weledi katika taaluma ya viwanja vya ndege aliiagiza bodi ya Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa ina ajili watu wenye uwezo ili kuweza kuongezea mapato.

“Awali jukumu la kujenga viwanja lilikuwa kwenu lakini hivi sasa limepelekwa Tanroad hii yote ni kutoka na mamlaka yenu kuwa na watumishi ambao hawana weledi hasa katika mambo ya mamlaka ya viwanja vya ndege,” alisema.

Kutokana na hali hiyo Mhandisi Kamwelwe alitoa angalizo kwa uongozi wa mamlaka hiyo wakati utakapofika kuajili watumishi ambao watakuwa na tija na mamlaka hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!