Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi Manispaa Morogoro mbaroni kwa rushwa
Habari Mchanganyiko

Watumishi Manispaa Morogoro mbaroni kwa rushwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich Matei
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro (TAKUKURU) imewapandisha kizimbani watuhumiwa wawili wa Serikali kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya Rushwa ikiwemo Uhujumu Uchumi na kughushi nyaraka na kubadilisha matumizi ya fedha za Serikali. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, Agripina Kamaze mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Cleonce Cleophace alidai mahakamani hapo kuwa Herman Msuha ambaye ni Ofisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro amepandishwa kizimbani kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Cleophace alidai kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa Juni 1 hadi Desemba 31, 2015 mtuhumiwa alishindwa kuondoa jina la mtumishi wa manispaa ambaye ni marehemu Julius Maliyanga kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi kwa kipindi tajwa hapo juu.

Aidha mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mshtakiwa huyo amefunguliwa kesi ya jinai namba120/2018 kwa kutumia mamlaka yake vibaya akiwa Ofisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro kitendo ambacho ni kosa chini ya kifungu cha sheria namba 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.

Hivyo alidai kuwa mshtakiwa huyo pia amepandishwa kizimbani hapo kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara ya jumla ya Sh. 2.5 milioni ambalo ni kosa chini ya kifungu namba 57 kifungu kidogo cha kwanza na 60 (1) ya sheria ya uhujumu uchumi.

Mshtakiwa huyo alikana makossa hayo na yupo nje kwa dhamana huku kesi hiyo itatatjwa tena mahakamani hapo Juni 19 mwaka huu.

Katika tukio la pili Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mkuu wa shule ya Sekondari ya Tubuyu, Henry Mbawala na Mwenyekiti wake wa bodi ya shule hiyo, Robert Leole wamefikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Mbele ya Hakimu Kamaze mwendesha mashata huyo alidai kuwa washtakiwa hao walipandishwa kizimbani kufuatia kughushi muhtasari wa kikao cha bodi ya shule wa tarehe 08/01/2018 na kuonesha kuwa kampuni ya Tweyambe Agricultural and General Enteprises Co. Ltd kuwa imeshinda zabuni ya ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo jambo ambalo si kweli.

Washtakiwa hao walikana kuhusika na makossa hayo na wapo nje kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo Juni 19 mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!