Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumiaji wa simu waondolewa hofu
Habari Mchanganyiko

Watumiaji wa simu waondolewa hofu

Watumiaji wa simu za mkononi
Spread the love

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaondolea hofu watumiaji wa mitandao ya simu wanaotaka kutumia huduma ya laini moja kwa mitandao yote kuwa hatawakosa huduma zinazotolewa na makampuni ya simu, anaandika Mwandishi Wetu.

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tehama, Mhandisi Nehemia Mwenisongole, alisema hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema huduma hiyo itakuwa ya hiari kwa watumiaji wa mitandao ya simu na itawasaidia kuondokana na kumiliki utitiri wa laini nyingi za simu na kutumia laini moja iliyobeba mitandao yote ya simu ambayo atahitaji kutumia.

“Ukiamua kuhamia kwenye mfumo huu wa kuunganishwa kutumia namba moja hakutakuwepo na madhara ya kuanza kuwaza kuwa wapo watu ambao nitawapoteza nikiingia huko,’’ alisema.

Aidha, amesema kuingia kwenye mfumo huo itasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mtandao mahali mtumiaji atakapokuwa na kumsaidia kutumia mtandao mwingine utakaokua unapatikana eneo husika.

Amesema walianza kuingia kwenye mfumo huo wa mawasiliano kuanzia Machi mosi mwaka huu, ambapo alisema mchakato wa kuhamia mitandao mingine kwa kutumia namba moja hautazidi siku mbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!