Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

‘Watu wasiojulikana’ wapiga hodi polisi

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

JESHI la Polisi Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kufanya msako kuwasaka watu waliofanya mauaji ya askari polisi aliyeokotwa juzi akiwa amefariki, anaandika Angel Willium.

Askari Charles Yanga mwenye namba X-G 475 hivi karibuni akiwa amefariki pembeni ya uzio wa kambi ya polisi Ukonga na mwili wake ulionekana kuwa na majeraha kwenye paji la uso huku sikio moja likiwa limekatwa.

Katika kufuatilia polisi wamegundua askari huyo ameuwawa na watu wasiyojulikana kisha kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua askari wanaodaiwa kuwapiga wananchi katika eneo la Gogo la Mboto jijini Dar es Salaam kwa madai ya kulipiza kisasi.

“Kama Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, jambo ambalo limefanyika kwa siku tatu hizo halikubaliki na kama kuna matatizo ya askari na raia kulikuwa kuna eneo la kupeleka matatizo hayo.”

Mnamo tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2017 majira ya saa 06:00 huko maeneo ya kambi ya polisi Ukonga jijini Dar es Salaam makao makuu mkoa wa kipolisi, askari walikuta mwili wa polisi nje ya kambi hiyo.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
JESHI la Polisi Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kufanya msako kuwasaka watu waliofanya mauaji ya askari polisi aliyeokotwa juzi akiwa amefariki, anaandika Angel Willium. Askari Charles Yanga mwenye namba X-G 475 hivi karibuni akiwa amefariki pembeni ya uzio wa kambi ya polisi Ukonga na mwili wake ulionekana kuwa na majeraha kwenye paji la uso huku sikio moja likiwa limekatwa. Katika kufuatilia polisi wamegundua askari huyo ameuwawa na watu wasiyojulikana kisha kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi. Aidha, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua askari wanaodaiwa kuwapiga wananchi katika eneo la Gogo la…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Angel Willium

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube