LICHA ya kuwa na namba za utambulisho wa uraia (NIDA), watu 3,000,000 hawajasajili laini zao za simu kwa alama za vidole. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).
James Kilaba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ametoa kauli hiyo tarehe 14 Desemba 2019, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia usajili wa laini za simu, Kilaba amesema utafiti unaonesha kuwa, mtu mmoja anamiliki laini zaidi ya moja na kwamba, katika idadi hiyo ya watu (3,000,000), wanatarajia kusajili laizi zaidi ya milioni 5.6.
Mpaka kufika tarehe 10 Desemba 2019, laini za simu zilizosajiliwa nakutambuliwa na TCRA ni 47,063,603. Laini hizo zinamilikiwa na watu milioni 21.1.
Lakini laini zilizosajiliwa kwa njia ya alama za vidole ni 19,681,06 sawa na asilimia 42. Laini hizo zinamilikiwa na watu 7.6.
Leave a comment