JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu 45 kwa tuhuma mbalimbali pamoja na kukamata silaha, mali za wizi na madawa ya kulevya katika maeneo, anaandika Dany Tibason.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Kamishina mwandamizi msaidizi wa Jeshi la Polisi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa kutokana na msako unaoendelea kufanywa na Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao katika matukio tofauti.
Leave a comment