Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Watu 188 wahofiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya ndege
Kimataifa

Watu 188 wahofiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya ndege

Spread the love

WATU takribani 188 wanahofiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya ndege ya abiria ya Shirika la Lion Air iliyokuwa safarini kutoka mji mkuu wa Indonesia, Jarkata kuelekea mji wa Pangkal Pinang. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ndege hiyo yenye safari namba JT-610 iliyoondoka mjini Jakarta siku ya Jumatatu majira ya saa 06:20 (23:30 GMT Jumapili kwa saa za Afrika Mashariki) imeangukia baharini Baada ya kusafiri kwa muda mfupi.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 namba JT-610 kabla ya kuangukia baharini ilipoteza mitambo ya rada baada ya kupaa ilipokuwa inavuka bahari.

Msemaji wa Shirika la Huduma za Uokoaji na utafutaji wa manusura, Yusuf Latif amethibitisha kuhusu tukio hilo, na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

Naye Afisa wa Bandari nchini humo, Tanjung Priok amesema shughuli za uokoaji manusura zimeanza ambapo vyombo vya bahari ikiwemo boti na meli zimebeba waokoaji kuelekea eneo la tukio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!