Watoto 30 waibuliwa Iringa, kwenye shindano la kusaka vipaji

Spread the love

KITUO cha kukuza vipaji cha Iringa Football Academy kimefanya majaribio ya wazi (Trial) kwa watoto wenye umri wa miaka 15 mkoani humo na kufanikiwa kuapata watoto 30 wenye vipaji vya mpira wa mpira wa miguu na kuwaendeleza. Anaripoti Mwandishi wetu… endelea

Majaribio hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Samora na kujitokeza jumla ya watoto 152 ambao walikuwa wanatafuta nafasi kwenye kituo hicho.

Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Ally Msigwa amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kuwatafuta watoto wenye vipaji halisi na kuviendeleza licha ya kukutana na chagamoto ya udanganyifu wa umri kwa wachezaji wengi na kuamua kuanza upya.

“Hapo kabla kituo kilikuwa na watoto chini ya miaka 20 nikaja kugundua watoto wengi walikuwa wamedanganya umri nikaamua kuanza upya na nimeamua kuanza na watoto chini ya miaka 15” alisema mkurugenzi huyo

Kwa upande wake mwalimu wa kituo hicho Salehe Moleli amesema kuwa vijana wengi mkoni humu wana vipaji ila wamezoea kucheza bila kusimamiwa na walimu.

“Watoto wengi ni vijana wadogo na wamezoea kucheza mchangani bila kusimamiwa na walimu hivyo hapa tumewaona wengi wanavipaji lakini wanawoga lakini tunaahidi tutawapa mazoezi na tutawatoa woga”alisema kocha huyo

“Natoa wito kwa TFF kuwaona vijana wenye vipaji na kuwaendeleza ili kukuza vipaji vyao,ili tuwe na taifa lenye vipaji lakini changamoto kubwa ni vifaa na fedha” aliongezea Salehe Moleli

Nasri Swai  mmoja wa watoto waliopita katika usaili huo alisema anandoto ya kuwa mchezaji mkubwa kama samatta na atahakikisha anatimiza ndoto zake.

“Mimi natamani kuchezea timu kubwa nifahamike kama Samatta na ninatarajia kupitia kipaji change nitawasaidia vijana wengine kufikia malengo yao”

 

KITUO cha kukuza vipaji cha Iringa Football Academy kimefanya majaribio ya wazi (Trial) kwa watoto wenye umri wa miaka 15 mkoani humo na kufanikiwa kuapata watoto 30 wenye vipaji vya mpira wa mpira wa miguu na kuwaendeleza. Anaripoti Mwandishi wetu... endelea Majaribio hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Samora na kujitokeza jumla ya watoto 152 ambao walikuwa wanatafuta nafasi kwenye kituo hicho. Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Ally Msigwa amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kuwatafuta watoto wenye vipaji halisi na kuviendeleza licha ya kukutana na chagamoto ya udanganyifu wa umri kwa wachezaji wengi na kuamua kuanza upya. “Hapo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!