Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watengenezaji vinywaji vya Energy waonywa
Habari Mchanganyiko

Watengenezaji vinywaji vya Energy waonywa

January Makamba, Waziri wa Nishati
Spread the love

JANUARI Makamba, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mazingira na Muungano ametoa angalizo kwa watengenezaji wa vinywaji vya Enegy kwamba, chupa zake hazidhibitiki. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Aprili 2019 amesema, takataka aina ya chupa zimekuwa ni ajira kwa waokotaji na kuwa, serikali imepanga kurasimisha shughuli hiyo lakini chupa za Energy hazinunuliki.

Amewataka watengenezaji wa chupa za vinywaji hivyo kutafute namna ya kuzifanya ziwe kwenye mzunguko wa kutoka kwenye mazingira kama takataka.

“Washiriki kuziondoe katika mazingira, wewe unatengeneza Enegy Drink ukaamua kuzipiga rangi, hujui chupa inakwenda wapi na halafu hujui namna ya ile chupa inaweza kurudishwa,” amesema Makamba.

Amesema kuwa, serikali inajianda kisera kuhakikisha kuwa, takataka zinakuwa mali zenye kutoa fursa ya kiuchumi nchini.

Akizungumzia fursa itokanayo na takataka za chupa amesema kuwa, imetoa ajira kwa watu wanaoziokota na kwenda kuuza ambapo serikali imepanga kuwatambua rasmi watu hao.

“Watu wanakusanya taka tunaona wanazunguka na wakati mwengine tunawaona kama vichaa kwasababu wanaokota makopo, lakini ile ni shughuli ya kipato, sisi tunaona irasimishwe.

“Miji mingi dunini na hata hapa kwetu, kulingana na shughuli za uchumi, uzalishaji taka unazidi kukua hivyo serikali tunalitazama hilo kwenye kutengeneza mifumo ya kuzifanya kuwa mali.” amesema.

Na kwamba, mfumo wa utupaji wa taka na urejeshaji wake ni muhimu ukapangiliwa ili kuleta manufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!