July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watatu mbaroni tuhuma mauaji ya dereva tax Dar

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Dar es Salaam

Spread the love

POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva tax (UBER), Joseph Tillya Mpokala,(51),Mkazi wa Mbezi kwa Msuguli. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao ni, Godson Mzaura,(29),Mkazi wa Mbezi Beach,Mpiga picha, Said Mohamed Mahadhi (38),Mkazi wa Afrikana,Fundi simu na Denis Urassa (45),Mkazi wa Makongo Juu,Fundi simu.

Katika taarifa yake kwa umma, aliyoitoa leo Jumatano tarehe 3 Juni 2020, Mambosasa amesema, tarehe 25 Mei 2020 26.05.2020 walipata taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa mme wake ametoweka tangu tarehe 21 Mei 2020 na simu zake zote hazipatikani.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salam kupitia kikosi chake cha kupambana na uhalifu, kilianza ufuatiliaji mara mmoja.”

“Mnamo tarehe 27 Mei 2020 alikamatwa mtuhumiwa Godson Mzaura na kuhojiwa kisha kukiri kufanya mawasiliano na marehemu ambapo alieleza tarehe 21 Mei 2020 saa saba mchana, walimkodi marehemu ili awapeleke maeneo ya Mbezi na walipofika Mbezi Juu, watuhumiwa hao walimuua Joseph Tillya na kumfukia kwenye shimo katika eneo la wazi lenye uzio wa ukuta ambao hujamalizika kujengwa(pagale),” amesema Mambosasa

Amesema, jana Jumanne tarehe 2 Juni 2020, “watuhumiwa wote watatu walihojiwa kwa kina na kukiri walifanya mauaji hayo na kuchukua gari la marehemu lenye namba T 139 DST Toyota IST na kwenda kulificha huko Kimara Baruti katika nyumba ya wageni ya Api Forest logde.”

Mambosasa amesema, wanakamilisha taratibu za kupeleka jalada kwa mwasheria wa serikali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

error: Content is protected !!