Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania waishi kama wakimbizi nchini mwao
Habari MchanganyikoTangulizi

Watanzania waishi kama wakimbizi nchini mwao

Spread the love

FAMILIA ya watu 19 imeeleza namna inavyolala chini ya mti baada ya nyumba yao kubomolewa katika operesheni ya kuwaondoa wafugaji iliyofanyika Loliondo, Ngorongoro, mkoani Arusha, anaandika Nasra Abdallah.

Baba wa familia hiyo Musa Sereti (34), ameelezea jinsi alivyoathirika na operesheni hiyo iliyofanyika kwa takribani miezi mitatu kabla ya kusitishwa na Waziri Wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala.

Sereti ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ololosokwani, ambacho ni kimojawapo kilichoathirika na operesheni hiyo, anesema hali hiyo inawasababisha yeye na watoto wake 15 na wake zake watatu kuishi katika hali ya hofu huku wakijifunika na turubai.

Mkazi huyo amesema hali ikiwa mbaya zaidi pale mvua inaponyesha na kujikuta wakikesha kwa ajili ya kujikinga na mvua na kuangalia watoto ambao kwao ni rahisi kiugua kutokana na kunyeshewa mvua.

“Mimi sikuwa na maisha haya, nilikuwa ni mtu nina maboma yangu na watoto wangu waliweza kuishi kwa raha mustarehe, lakini kufanyika kwa operesheni hii kumenifanya nimi na familia yangu tuishi kama wakimbizi kwenye nchi yetu,” amesema Sereti.

Akielezea kuhusu hali ya uchuni, Sereti amesema hivi sasa amejikuta akifanya manunuzi ya bei kubwa ukilinganisha na huko nyuma kutokana na mazingira magumu wanayoishi na wakati mwingine hata upatikanaji fedha ni mgumu.

Amesema awali manunuzi ya bidhaa za nyumbani yalikuwa yanapungua kutokana na kuwa na mifugo, ambapo aliweza kupata maziwa kwa ajili ya watoto lakini sasa analazimika kuyanunua na hivyo kuongeza gharama ya matumizi za maisha.

Kwa upande wake mmoja wa wake wa Musa, Nasarati Sereti, amesema kwao chakula kikuu kwa watoto ili wakue vizuri na akili ni maziwa, lakini kutokana na halo ngumu inawabidi wawalishe uji usiokuwa na chochote.

Familia hiyo wakiwa ndani ya hema dogo wanapoishi kama nyumba yao

Pia mama huyu amesema hata ule wasaa wa faragha na mume wao umekuwa mgumu kwao kutokana na kuishi wote eneo moja tofauti na ilivyokuwa kabla ya operesheni ambapo kila mmoja alikuwa na nyumba yake.

Operesheni ya kuwaondioa wafugaji katika Tarafa hiyo ya Loliondo ilianza Agosti 13, ambapo mbali na kukamatwa kwa mifugo yao pia kuliambatana na kuchomewa maboma yao na kuwaacha wengi wakiwa hawana mahala pa kuishi na kupoteza mali zenye thamani ya mamilioni.

Tukio hilo la uchomaji linaelezwa kufanywa na polisi wa Longido wakishirikiana na wale wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, (SENAPA) pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, (NCAA) huku Vitongoji zaidi ya 14 vikiwa vimeathirika

Chanzo cha mgogoro huo kimetokana na Mamlaka hizo za Hifadhi, kutaka kumega eneo la kilometa 1500 katika vijiji hivyo na kupafanya rasmi pori tengefu litakalounganishwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!