Wasimamizi wakiwa katika majukumu yao kwenye moja ya kituo cha kupigia kura nchini

Watanzania kuamua, mawakala tatizo  

Spread the love

WATANZANIA milioni 29.8 waliojiandikisha katika daftari la kudumumla wapiga kura wanaendelea na shughuli ya upigaji kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Wanaripoti Waandishi Wetu … (endelea).

Shughuli hiyo ya upigaji kura imeanza saa 1:00 asubuhi na inatarajiwa kuhitimishwa saa 10:00 jioni katika jumla ya vituo vya kupigia kura 80,155 nchini humo.

Wagombea 15 wa nafasi ya urais wanachuana kwenye nafasi hiyo huku wagombea wawili Rais John Pombe Magufuli wa CCM na Tundu Lissu wa Chadema wanapewa fursa kubwa kuibua washindi.

Majimbo 264 ya uchaguzi wanachuana huku CCM tayari imejikusanyika majimbo 28 baada ya wagombea wao kupita bila kupingwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa sababu kadhaa.

Katika maeneo mbalimbali nchini, hali ya upigaji kura inaendelea huku kukiwepo changamoto kadhaa ikiwemo ya baadhi ya wapiga kura, kutokuona majina yao.

Mgombea Ubunge wa Tarime Vijijini Mkoa wa Mara kupitia Chadema, John Heche amesema, mawakala wake wengi wamekamata na polisi.

Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, katika kituo cha Kwa Jofu, , Riziki Msafiri amezungumza na MwanaHALISI Online akisema “mimi nimefika hapa ambapo nilijiandikisha lakini jina langu sijalikuta. Sijajua imekuwaja sasa.”

Naye Regina Mkonde aliyefika kituo cha Chakula Bora katika Shule ya Sekondari Manzese, Dar es Salaam amesema “hakuna shida, utarartibu wa foleni ulikuwa mzuri, vituo vimepangwa kwa herufi, kwa kifupi hali ilikuwa shwari na nimepiga kura yangu vizuri kabisa.”

Baadhi ya changamoto ni mawakala wa vyama kutokupata fursa ya kuingia kutekeleza wajibu wao kwa kutokuwa na utambulisho unaomwezesha kuwakilisha wagombea wao.

Changamoto hiyo, imejitokeza maeneo mbalimbali hususan mawakala wa vyama vya upinzani kulalamikia suala hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akizungumza katika moja ya kituo cha kupigia kura amewaonya wale wote wanaotarajia kufanya vurugu watachukuliwa hatua kali bila kujali “kama wewe ni diwani au mbunge.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

WATANZANIA milioni 29.8 waliojiandikisha katika daftari la kudumumla wapiga kura wanaendelea na shughuli ya upigaji kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Wanaripoti Waandishi Wetu … (endelea). Shughuli hiyo ya upigaji kura imeanza saa 1:00 asubuhi na inatarajiwa kuhitimishwa saa 10:00 jioni katika jumla ya vituo vya kupigia kura 80,155 nchini humo. Wagombea 15 wa nafasi ya urais wanachuana kwenye nafasi hiyo huku wagombea wawili Rais John Pombe Magufuli wa CCM na Tundu Lissu wa Chadema wanapewa fursa kubwa kuibua washindi. Majimbo 264 ya uchaguzi wanachuana huku CCM tayari imejikusanyika majimbo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!