Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Watanzania jiungeni na bima’
Habari Mchanganyiko

‘Watanzania jiungeni na bima’

Spread the love

WATANZANIA wameshauri kuwa na utamaduni wa kukatia bima nyumba, viwanda na gari zao hatua itakayosaidia kurejeshewa baadhi ya mali pindi zitakapokumbwa na majanga ya moto na ajali za barabarani, anaandika Moses Mseti.

Agousti 15 mwaka huu, soko la Sido mkoani Mbeya liliteketea kwa moto na kusababisha mali za wafanyabiashara katika soko hilo kupoteza bidhaa na mali zao huku ikielezwa wafanyabiashara wengi hawakuwa na bima za bidhaa.

Ushauri huo umetolewa leo na Meneja wa Kanda ya ziwa wa Kampuni ya Bima ya Bumaco, Godlisten Muro, wakati wa kukabidhi hundi ya Sh. 140 kwa mmiliki wa mabasi ya Batco, ambaye basi lake liliteketea kwa moto Mei mwaka huu.

Amesema hiyo ni mara ya pili kwa kampuni yao kumlipa mfanyabiashara huyo baada ya mwaka juzi kumlipa kiasi cha Sh. 171 kitendo ambacho alidai bima yao inalenga kumrudishia mwanachama wao kiasi cha mali iliyokumbwa na majanga.

“Wananchi wengi nchini wanakatia bima baadhi ya mali kama gari wakiamini kwamba bima ni kwa ajili ya Polisi wa usalama barabarani au kwa mikopo ya benki ni lazima watu wawe na bima sokoni kwa usalama wa mali zao nyingine,” amesema Muro.

Muro amesema katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu iliyobaki watahakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha wanakata bima huku akidai wananchi walio wengi wamekuwa wakivunjika sehemu za mwili kwa ajali barabarani lakini hawafahamu na wao wanaweza kulipwa.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kanda ya ziwa, Sharifu Ally Hamad, amewataka watanzania kujiunga na bima ili wakati wanapopatwa na majanga ya moto na ajali waweze kuwa na uhakika wa kulipwa.

Hamad pia aliipongeza kampuni hiyo ya Bumaco kwa namna inavyolipa kwa wakati fidia wateja wao na kuwawataka wananchi wafanyabiashara kujiunga na mfumo wa bima  ili kunufaika na fidia zinazotolewa na makampuni mengine.

Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Batco, Baya Maragi amewasihi wafanyabiashara wenzake kujiunga na kampuni ya bima ya Bumaco kwa kuwa imekuwa ikimlipa kwa wakati madai yake ya bima, ambapo alikiri ni mara yake ya pili kulipwa madai yake ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!