Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Siasa Wapinzani wajibu mashambulizi Muswada Vyama vya Siasa
Siasa

Wapinzani wajibu mashambulizi Muswada Vyama vya Siasa

Baadhi ya wabunge wa Upinzani katika Bunge lililopita
Spread the love

MUSWADA wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya siasa umetua bungeni leo huku Kambi Rasmi ya Upinzani ikianisha hoja zake kupinga muswada huo. Anaripoti Tibason Kaijage…(endelea)

Akiwasilisha bungeni leo tarehe 29 Januari 2019, Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Ester Bulaya amesema, muswada huu sio rafiki kwa vyama vya siasa.

“Unaletwa bungeni huku wadau muhimu wa siasa kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mheshimiwa Esther Nicolaus Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Nje wakiwa gerezani yapata miezi miwili sasa.

“…Kabla hata ya kupitishwa kwa muswada huu, ambao kwa kiwango kikubwa unaharamisha na kufanya shughuli za kisiasa kuwa makosa ya jinai hapa nchini, tayari viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakiandamwa na kesi za kisiasa wakiwemo takriban viongozi wote wa juu wa CHADEMA, Kiongozi wa ACT Wazalendo Mheshimiwa Zitto Kabwe na Mheshimiwa Seleamani Bungala  – Mbunge wa Kilwa Kusini.

“Ni vema Serikali hii ya CCM ikatambua kwamba siasa ni mfumo unaogusa maisha ya watu moja kwa moja. Kwa sababu hiyo, inapoleta muswada kandamizi kama huu, madhara yake hayatavikumba vyama vya siasa peke yake ambavyo serikali imepanga kuvidhibiti, bali yataathiri maisha ya wananchi kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na hata wale wasio na vyama,” amesema.

Bulaya amesema, dhana kuu ya muswada huo ni kumpa msajili wa vyama vya siasa nguvu kubwa ya kuingilia uendeshaji wa vyama vya siasa na hadi kuwavua uanachama wanachana na viongozi wa vyama.

“Nguvu hii inapitiliza na inampa uwezo zaidi ya ule ambao Katiba za vyama zinautoa kwa wanachama na viongozi wake.

“Msajili ni mlezi wa vyama, katika hilo tulitarajia angalau alete muswada ambao utaweza kutatua mizozo baina ya viongozi ndani vyama, baina ya vyama na baina ya vyama na Serikali na au Tume ya Uchaguzi.”

Amesema kuwa, kuanzia mwanzo wa muswada katika vifungu vyote vinavyotoa adhabu, hakuna kifungu chochote kinachotoa haki ya kusikilizwa na haki ya kukata rufaa pale mhusika anapoona kuwa hakutendewa haki.

Tukumbuke kuwa haki ya kusikilizwa na kukata rufaa ni haki ya msingi kwa mhusika,”aamesema

Bulaya.amesema, kifungu cha 3(c) cha muswada huo kinatoa mamlaka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi wa ndani ya Chama, jambo ambalo linapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

“Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kifungu hicho kifutwe na badala yake msajili awe na jukumu la kukuza demokrasia na utawala bora ndani na miongoni mwa vyama vya siasa.

Kwa maana hiyo kifungu hicho kisomeke kama ifuatavyo: to promote democracy and good governance within and among political parties,” amesema Bulaya.

Akizungumzia uraia Bulaya amesema, elimu ya urai ni haki ya kila Mtanzania bila kujali kama ni mwanachama wa chama chochote cha siasa au la.

Amesema, elimu hiyo hutolewa kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi elimu ya juu ambapo kwa mantiki hiyo, hii siyo kazi ya msajili wa vyama vya siasa.

“Kwa kuwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Serikali kupitia wizara ya elimu na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Hata kama muswada huu ulimaanisha elimu ya mpiga kura, bado jukumu hilo lingekuwa chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na siyo Msajili wa vyama vya siasa.

“Kifungu cha 3(g) na kikisomwa pamoja na kifungu cha 5A vyote vinazungumzia kuhusu elimu ya uraia.

“Wakati kifungu cha 3(g) kinampa mamlaka Msajili wa Vyama vya siasa kudhibiti elimu ya uraia, kifungu cha 5A kinaweka masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia,” amesema.

Akizungumzia mamlaka ya msajili Bulaya amesema, kifungu kipya ya 5B cha muswada kinampa mamlaka makubwa msajili kutaka taarifa yoyote kutoka kwenye Chama au Kiongozi wa Chama.

Amesema, Kambi Rasmi ya Upinzani inapinga msajili kutaka taarifa yoyote kwani taarifa nyingine ni siri kwa ajili ya maslahi na ustawi wa chama.

“Mathalani haitakuwa afya chama cha siasa kikatakiwa kutoa taarifa ya mikakati yake ya kushinda uchaguzi na kuitoa kwa mamlaka za Serikali iliyoko madarakani.

Kwa hiyo, ni vema muswada huu ukaainisha aina taarifa zinazotakiwa kutolewa kwa msajili,”amesema.

  Amesema, kifungu kipya cha 6A(3) kinaingilia utaratibu wa Katiba za Vyama kwa kutoa sharti kuwa Mkutano Mkuu au Kamati Kuu visikasimu madaraka yake.

“Huku ni kuingilia utaratibu wa kawaida wa Vyama kwa mujibu wa katiba zao. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kifungu hiki hakileti afya kwa siasa za vyama vingi, hivyo kifutwe.

Pia Bulaya kagusia kifungu cha 6B (a) kinachoeleza kwamba, ili mtu aweze kusajili chama cha siasa, ni lazima wazazi wake wote wawili wawe ni raia wa Tanzania.

Amesema, kifungu hicho kinatoa taswira ya ubaguzi na kuonesha kuwa Tanzania kuna raia ambaye uraia wake ni wajuu kuliko wa mwenzake.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  tunaamini kuwa  kama  mtu ni raia wa Tanzania basi haina haja tena ya kuangalia  uraia wa wazazi wake. 

“Ibara ya 13 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema kuwa Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

Habari MchanganyikoSiasa

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waapishwa rasmi  

Spread the loveWABUNGE wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki...

HabariSiasa

Vigogo ACT mbaroni kwa uchochezi, kukashifu viongozi wa Serikali

Spread the loveJESHI la Polisi Mkoa wa Kusini limewakamata na kuwahoji watu...

HabariSiasa

Shaka CCM tusipoteze muda  wa malumbano

Spread the loveKATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi...

error: Content is protected !!