Wapiga debe waiangukia serikali – MwanaHALISI Online
DSC07012

Wapiga debe waiangukia serikali

ZAIDI ya vijana 200 ambayo wanaopiga debe eneo la Kamanga Ferry jijini Mwanza, wameiangukia serikali na kuiomba iwaache waendelee na shughulzao na kusitisha mpango wake wa kutaka kuwaondoa hapo, anaandika Moses Mseti.

Vijana hao wametoa kilio chao kwa Katibu wa Umoja na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Mwanza, Mariam Amiri.

Mwenyekiti wa wapiga debe hao, Husein Manyika, amesema baada ya kusikia tangazo la serikali kupitia vyombo vya habari ambalo linawataka kuondoka na kuacha kazi hiyo, limewashtua na kwamba hawajui pa kwenda.

Amesema kuwa katika eneo hilo pia wapo wapiga debe, wachuuzi wa samaki pamoja na wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga.

“Tunaambiwa tuondoke hapa (Kamanga), wakati serikali haijatuandalia maeneo ya kutupeleka hivyo kabla hawajatuondoa, wanapaswa kukaa na watafakari ni wapi watakapotupeleka ndipo wachukue uamuzi huo,” amesema Manyika.

ZAIDI ya vijana 200 ambayo wanaopiga debe eneo la Kamanga Ferry jijini Mwanza, wameiangukia serikali na kuiomba iwaache waendelee na shughulzao na kusitisha mpango wake wa kutaka kuwaondoa hapo, anaandika Moses Mseti. Vijana hao wametoa kilio chao kwa Katibu wa Umoja na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Mwanza, Mariam Amiri. Mwenyekiti wa wapiga debe hao, Husein Manyika, amesema baada ya kusikia tangazo la serikali kupitia vyombo vya habari ambalo linawataka kuondoka na kuacha kazi hiyo, limewashtua na kwamba hawajui pa kwenda. Amesema kuwa katika eneo hilo pia wapo wapiga debe, wachuuzi wa samaki pamoja na wafanyabiashara wadogo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Moses Mseti

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube