Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waombaji 25,000 wakosea kuomba mkopo Elimu ya Juu
Habari Mchanganyiko

Waombaji 25,000 wakosea kuomba mkopo Elimu ya Juu

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu
Spread the love

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka waombaji mikopo katika mwaka wa masomo 2018/2019 ambao fomu zao zina kasoro, kurekebisha kasoro hizo ndani ya siku saba kuanzia Septemba 24 hadi 30, 2018 ili wapangiwe mikopo. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na HESLB, inaeleza kwamba zaidi ya waombaji 25,000 katika maombi ya mikopo 78,833 yaliyopokelewa Julai 31, 2018 , fomu zao zilibainika kuwa na upungufu wa nyaraka na uthibitisho wa kuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya kupangiwa mikopo katikati ya mwezi Oktoba, mwaka huu.

HESLB imewataka waombaji hao kupitia majina yao kwenye orodha iliyowekwa katika tovuti ya bodi hiyo, kisha kuingia kwenye mtandao wa maombi ya mikopo ili kufanya masahihisho kwa kufuata hatua zilizowekwa na baada kukamilisha, waziwasilishe ndani ya muda uliopangwa bila kutuma tena kwa njia EMS .

“Kwa taarifa hii pia tunapenda kuwakumbusha waombaji wa mikopo ambao wamo katika orodha hiyo yenye upungufu wa taarifa kusoma kwa umakini na kurekebisha kasoro hizo ili waweze kupangiwa mikopo. Aidha tunawatahadharisha dhidi ya matapeli wanaoweza kutumia taarifa hiI kuwalaghai waombaji mikopo kuwa wanaweza kuwasaidia kupata mikopo. Tangazo maalum na mwongozo wa marekebisho vinapatikana katika tovuti hii,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kusoma majina ya wanafuzi wanaotakiwa usahihisho ingia hapa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!