Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanawake wapigiwa debe kugombea nafasi Serikali za Mtaa
Habari za Siasa

Wanawake wapigiwa debe kugombea nafasi Serikali za Mtaa

Spread the love

WANAWAKE mkoani Morogoro wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu huku wakijitathmini wenyewe na kujiona wanatosha badala ya kusubiri kubebwa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Ushauri huo ulitolewa jana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake juu ya nafasi ya mwanamke katika uongozi ambapo alisema, wanawake wanapaswa kutumia fursa iliyopo kufuatia kuwa chama bado kinaimani na wanawake kutokana na wanawake walioko kwenye uongozi kuendelea kuonesha kazi nzuri.

“Si wakati wa kubebwa wenyewe wajibebe, waache makundi ambayo hayana msingi, waache tabia za kusindikiza watu yaani kuwabeba na sasa mtu ajitathmini akijiona anatosha aende mwenyewe,” alisema Shaka.

Alisema, kazi ya kuhamasisha kina mama inakwenda vizuri na kwamba suala la uongozi ni maamuzi ya mtu mwenyewe kuamua kufuatia CCM kuwa na mfumo kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, wilaya, mkoa na Taifa ambapo ngazi zote zinaendelea kufanya kazi kwa kuwapatia taaluma ya itikadi ya chama, uzalendo na utayari katika kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao.

Aidha Shaka alisema, uwiano wa mwaka 2014 katika chaguzi za mitaa na vitongoji kwa asilimia kubwa wakinamama walijitokeza huku waliopata fursa ushiriki wao ulikuwa mzuri katika usimamizi, ufuatiliaji, uwajibikaji  na kuona namna ilani ya CCM inatekelezwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo yao.

Hivyo alisema, wana imani kubwa mwaka 2019 idadi ya kinamama watakaojitokeza kugombea itakuwa ni kubwa zaidi ukilinganisha na mwaka 2014 sambamba  na chama kuwa kimeweka msimamo mzuri wa kuona kunakuwa na uwiano wa wanawake, vijana na makundi mengine kupitia jumuiya tatu zilizopo ambazo ni vijana wanawake na wazazi ambao wote wanajukumu la uhamasishaji.

Katibu huyo alisema, hatua pekee ya kumshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli ni kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili kumpa ushindi mkubwa na wa kishindo ambao utamuongeze nguvu kwa kuona kwamba viongozi wengi wa mitaa wamepita kwa wingi kutoka CCM.

Hata hivyo alisema kwa sasa wamekuja na kauli mbiu ya Morogoro ya kijani ambayo itakuwa na kauli mbiu ya kwamba ‘tuwe pamoja tusikubali kugawanyika’ kwa sababu wanaamini kuwa hata uchaguzi wa mwaka 2015 walipoteza viti vya mitaa katika maeneo kwa bahati mbaya.

“Lengo la Moro ya kijani ni kuhakikisha kuwa hatufanyi tena makosa yale ya 2014 na tusikubali kugawanyika kwa namna yoyote sababu maumivu tuliyopata 2014/15 yalitokana na wana CCM wenyewe kwa asilimia kubwa kwa huo mgawanyiko tuliosema, lakini sasa 2019/20 tusigawanyike maana sote tunajua kwamba mfumo wa chama tunakwenda kwenye ushindani kuanzia kwenye kura za maoni,” alisema.

Alisema, kufuatia kampeni na mifumo iliyopo wanauhakika wa kuongeza uwiano wa wanawake na kuongeza kura kwa asilimia 99.9 za Rais Magufuli kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!