SAKATA la malipo ya fidia kwa wakazi wanaopisha mradi wa bomba la mafuta vijiji vya Kata ya Chongoleani, limeingia sura mpya baada ya wadau wa Asasi za kiraia mkoani hapa kushinikiza haki itendeke kwa wananchi hao ili walipwe kabla ya mradi huo kuanza, anaandika Mwandishi Wetu.
Aidha, serikali na Asasi za kiraia zimetakiwa kuwaandaa wananchi katika kukabiliana na changamoto za uwekezaji ili wazawa wasiwe wasindikizaji kwenye uchumi.
Mkutano huo uliofunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella ulihusu kujenga ushirikiano na kuaminiana baina ya Asasi za kiraia na serikali.
Wakichangia katika mkutano huo wananchi wanaopisha mradi huo waliitaka serikali kuwasikiliza madai ya wananchi hao badala ya kuwapuuza.
Leave a comment