Wananchi wahimizwa kuwekeza kwenye hisa – MwanaHALISI Online
Mkurugenzi wa Bodi ya TCCIA, Donald Kamori
Mkurugenzi wa Bodi ya TCCIA, Donald Kamori

Wananchi wahimizwa kuwekeza kwenye hisa

WANANACHI wametakiwa kuhudhuria semina zinahusua uwekezaji wa hisa ili wapate elimu itakayowasaidia kupata ufahamu kwa undani kuhusu biashara hiyo endelevu, anaandika Angel Willium.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA Investment, Arphaxad Masumbu wakati wa kuanzimisha miaka 12 ya wanahisa nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Masumbu amesema wanachangamoto ya kutokuwa na watu wengi katika ununuaji wa hisa, hilo linatokana na wananchi kutokuwa na elimu juu ya biashara hiyo yan uwekezaji.

“Mikoani kumekuwa na mwitikio mdogo, wakushiriki semina za elimu kwa wananchi, hivyo tunaingia gharama kubwa kuandaa mikutano, watu hawajui kwamba biashara ya kununua na kuuza hisa ni endelevu kwani usipofaidika wewe basi itamsaidia mtoto wako,” amesema Masumbu.

Naye Mkurugenzi wa bodi ya TCCIA, Donald Kamori amesema wameimalisha mtaji wao ambao kwa sasa umefikia Tsh. 1.28 bilioni kutoka 1.9 bilioni, fedha hizo wamewekeza kwenye makapuni mbalimbali kama bank NMB na mengineyo.

TCCI Investment imeazimisha miaka 12 ya tangu kuanzishwa mwaka 2005, mwaka jana waliweza kutekeleza majukumu ya kusimamia zoezi la kuthaminisha mali za kampuni.

WANANACHI wametakiwa kuhudhuria semina zinahusua uwekezaji wa hisa ili wapate elimu itakayowasaidia kupata ufahamu kwa undani kuhusu biashara hiyo endelevu, anaandika Angel Willium. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA Investment, Arphaxad Masumbu wakati wa kuanzimisha miaka 12 ya wanahisa nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Masumbu amesema wanachangamoto ya kutokuwa na watu wengi katika ununuaji wa hisa, hilo linatokana na wananchi kutokuwa na elimu juu ya biashara hiyo yan uwekezaji. “Mikoani kumekuwa na mwitikio mdogo, wakushiriki semina za elimu kwa wananchi, hivyo tunaingia gharama kubwa kuandaa mikutano, watu hawajui kwamba biashara ya kununua…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Angel Willium

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube