MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimesababisha madhara makubwa katika baadhi ya maeneo, ikiwamo watu kupoteza maisha na kutokuwa na makazi.
Hata hivyo, kumekuwapo na madai kuwa serikali imetimiza majumu yake kwa kuwataka wananchi waishio mabondeni kuhama katika maeneo wanayoishi.
Aidha, serikali na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatuhumu wananchi kuwa wamekuwa wakaidi mno wa kutuoondoka kwa maeneo yao.
Kumekuwapo na hata madai kuwa serikali imetoa viwanja kadhaa pembezoni mwa jiji kwa wananchi, lakini wananchi hawavitaki viwanja hivyo.
Si hivyo tu: Kumekuwapo na maneno kuwa jiji la Dar es Salaam, limejaa na halina tena nafasi ya kupokea watu wengine zaidi.
Napenda kueleza yafuatayo:
Dar es Salaam halijaja. Iimejazwa kutokana na mipango mibovu ya serikali ya CCM. Iimejezwa kwa sababu ya mchoko wa mawazo wa viongozi walioko madarakani.
Iimejezwa kutokana na ubinafsi, upendeleo na undumilakuwili wa CCM na serikali yake. Basi.
Nenda pale bonde la Msimbazi ambako maji yote yanayotoka Tabata, Pugu, Kisukulu, Kigogo, Mabibo, Kimara, Buguruni na maeneo mengine ya jiji, ukajionee jinsi maji yalivyozuia na kuta za viwanda zilizojengwa pembezoni mwa mikondo ya maji kwa ruhusa ya serikali.
Nenda Bonde la Msimbazi, eneo la Sukita ukaone jinsi lilivyobinafishwa na CCM kwa muwekezaji feki na ambaye amejenga ukuta unaozuia maji kutililika kuelekea baharini.
Angalia wananchi wanaoteseka kutokana na uroho huu wa fedha wa viongozi wao.
Hatua ya ujenzi huo, imeababisha mafuriko na uhalibifu mkubwa wa nyumba za watu.
Wananchi wamepigia kelele sana mipango mibovu ya ujenzi inayosimamiwa na kuratibiwa na serikali.
Hata hivyo, hakuna hatua zinazochukuliwa kwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliojenga katika maeneo hayo, ama ni wafadhili wa moja kwa moja wa CCM; na au baadhi ya viongozi wake.
Kwa muktadha huo, anayepaswa kulaumiwa katika hili, siyo wananchi. Ni serikali.
Saed Kubenea,
Mbunge wa Ubungo
Leave a comment