Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanakijiji wachanga Mil 20 kujenga madarasa
Habari Mchanganyiko

Wanakijiji wachanga Mil 20 kujenga madarasa

Spread the love

JUMLA ya Sh. 20 milioni zimetenwa na wanakijiji wa kijiji cha Mlilingwa, Ngerengere mkoa wa  Morogoro walizokusanya kutokana na mapato ya mkaa endelevu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya mkondo yatakayosaidia wanafunzi wanaotoka mbali. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mlilingwa, Pendo Masalu alisema analishukuru Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) kupitia mradi wake wa kuleta maeuzi katika sekta ya mkaa Tanzania (TTCS) kuwasaidia kielimu na kuweza kuchoma mkaa kwa njia endelevu ulioweza kuwaongezea kipato.

Alisema ujenzi wa madarasa hayo mawili ya mkondo utasaidia wanafunzi hasa wadogo wa chini ya miaka 7-8 wa darasa la kwanza na awali ambao hutembea umbali wa zaidi ya kilomita tisa kutoka nyumbani kwao jambo ambalo linakuwa shida kwao.

Alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifika shuleni saa tatu na kukuta masomo ya vipindi vya mwanzo yameshapita ambapo madarasa hayo yakishakamilika yatawasaidia watoto hao.

Nao wakazi wa kijiji hicho akiwemo Issa Mohamed alisema anashukuru kupata mradi huo kwani umewasaidia mambo mengi ikiwemo kuwapatia elimu watoto wao katika mazingira bora.

Mohamed alisema wamefaidika na mradi huo na mpaka sasa wameanzisha majengo mawili katika shule ya mkondo kwenye kijiji cha Ruvumo kilichopo katika tarafa hiyo.

Alisema wanafunzi wanapata adha kubwa hasa wakati wa masika kufuatia maji kujaa kwenye makorongo na kushindwa kufika shule kupata elimu na hivyo kushuka kitaaluma.

Kijiji cha Mlilingwa kinavyotekeleza mradi wa mkaa endelevu kupitia TTCS kwa ushirikiano na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia Tanzania (TaTEDO) kupitia Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa, kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!