Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 32, Walimu 2 mbaroni kwa tuhuma za kuchoma moto shule
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 32, Walimu 2 mbaroni kwa tuhuma za kuchoma moto shule

Spread the love

WATU 41 wakiwemo wanafunzi 32 na walimu wawili,  wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuhusika katika matukio ya shule kuchomwa moto. Anaripoti Regina Mkonde, Dar Es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 21 Desemba 2020 na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Liberatus Sabas wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama nchini.

Kamanda Sabas amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika nyakati tofauti.

“Katika matukio haya, wako watu wamekamatwa kuhusiana na matokio hayo, wanafunzi 32, walimu wawili, walinzi wawili, wengineo 5 jumla ya watu waliokamatwa ni 41,” amesema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas amesema watuhumiwa wengi katika sakata hilo ni wanafunzi, kwa kuwa  shule nyingi zimechomwa moto kutokana  na migogoro katika shule husika.

“Wengi ni wanafunzi sababu, ukiacha hitilafu ya umeme, matukio mengi yameonekana kusababishwa na wanafunzi wenyewe, aidha kutokana na migogoro iliyoko shule husika ambapo baadhi yao wameonesha kutokubaliana na mambo fulani fulani shuleni kwao. Na wengine kushawishiwa na baadhi ya watu,” amesema Kamanda Sabas.

Akielezea taarifa ya uchunguzi wa awali kuhusu matukio hayo, Kamanda Sabas ametaja chanzo cha shule hizo kuunguzwa ni, migogoro shuleni, hitilafu ya umeme na uzembe.

“Uchunguzi uliofanyika kuhusu sababu za shule hizo kuungua tumebaini yafuatayo, hitilafu ya umeme katika matukio 11, matukio ambayo yametokana migogoro shuleni ni 10, kuna tukio moja limetokana na uzembe ambayo uchunguzi unaendelea na mwisho wa siku tutatoa taarifa baada ya uchunguzi kukamilika,” amesema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas amesema matukio hayo yalikuwa 31 katika shule 28, ambapo shule za Serikali ni 11 na za taasisi ya dini na binafsi 17.

“Hivi karibuni kumezuka wimbi la uchomaji shule, mwaka 2019 matukio ya yalikuwa  kidogo kutokana na hitilafu ya umeme,   lakini mwaka huu tumeshuhudia matukio ya kuchoma shule ambayo yanafikia 31. Shule zilizoungua moto 17 ni za  taasisi za dini na binafsi, 11 za Serikali,  jumla ni shule 28,” amesema Kamanda Sabas.

Miongoni mwa shule zilizochomwa moto ni, Byamungu Islamic iliyoko Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera. Shule ya Awali na Msingi ya Taasisi ya Kiislamu ya Istiqama mkoani Tabora. Na Mivumoni Islamic Seminary, Ilala Islamic Seminary, Kinondoni Muslim,  za Dar Es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!