BARAZA Mitihani la Tanzania (Necta), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 215, waliofanya udanganyifu katika mitihani yao ya Taifa mwaka 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 15 Januari 2021, na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, wakati akitangaza matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne, darasa la nne na kidato cha pili jijini Dar es Salaam.
“Kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganyifu, watahiniwa 77 ni wa darasa la nne, 63 ni wa kidato cha Pili na 75 ni wa Kidato cha nne,” amesema Dk. Msonde
Pia, Dk. Msonde amesema, baraza hilo limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 252 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.
“Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2021 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.”
“Kati ya watahiniwa waliopewa fursa ya kurudia mitihani yao mwaka 2021, watahiniwa 17 ni wa kidato cha Pili na 235 ni wa kidato cha nne.
Leave a comment