Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 101 ‘wapigwa’ mimba Januari – Juni
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 101 ‘wapigwa’ mimba Januari – Juni

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

WIMBI la Wanafunzi wa kike Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kupewa mimba limezidi kuongezeka, baada ya Wanafunzi 101 kupewa mimba ndani ya miezi sita kwa mwaka huu, anaandika Moses Mseti.

Juni 6 mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alikuwa Lugalo jeshini alisema mtu yeyote atakaebainika amemkatisha masomo mwanafunzi wa kike kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jera.

Wanafunzi hao wa shule za msingi na sekondari walipewa mimba  katika kipindi cha kuanzia junuari mpaka Juni mwaka huu huku watu wanaotajwa kufanya vitendo hivyo ni baadhi ya madiwani, viongozi ngaji ya vijiji na watu wengine.

Tatizo la wanafunzi hao wa kike kupewa mimba liliibuliwa na Frank Bahati, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, baada ya kupata taarifa kwamba kuna mwanafunzi (jina linahifadhiwa) kisiwa cha Ukara anaujauzito na kuanza kufanya uchunguzi na kubaini ni kweli.

Hata hivyo, baada ya mkurugenzi huyo kupata taarifa za mwanafunzi huyo, alianza mara moja kufanya oparesheni katika wilaya hiyo na kubaini kuna wanafunzi wengine waliokatisha masomo kutokana na kupewa mimba.

Bahati akizungumza mara baada ya kuendesha msako wa kuwakamata wanafunzi, wazazi na watu waliowapa mimba wanafunzi hao, alisema katika miaka miwili iliopita (2015 – 2016) wanafunzi 250 walipewa ujauzito.

Amesema kuwa ripoti katika ofisi yake, zinaonesha idadi ya wanafunzi wa kike kupewa mimba ni kubwa na kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni viongozi waliopewa dhamna ya kusimamia sheria lakini anashangazwa kuona vitendo hivyo vikiwahusisha.

“Tatizo hili la wanafunzi wa kike kupewa ujauzito linachangiwa na Wazazi na serikali ya vijiji, kwa sababu hata nilipofika Irugwa (kata) nilikosa ushirikiano kutoka kwa viongozi na wazazi ambao mtoto wao amepewa mimba hali hii inasababisha ushahidi kukosekana.

“Wanafunzi 250 waliopewa mimba ni wa miaka miwili iliopita, hivi kuna wengine wamejifungua lakini hawa 101 ni wa mwaka huu pekee, hali hii inachangia kiwango cha elimu katika wilaya yetu kushuka kutokana na wanafunzi kupewa mimba,” amesema Bahati.

Hata hivyo, Bahati amesema sababu za wazazi, kushiriki kuficha taarifa za watoto wao waliopewa ujauzito ni kutokana na kupewa fedha huku akidai kwamba mtu yeyote atakaehusika kumpa mimba mwanafunzi hatua zitachukuliwa na kufikishwa kortini.

Francis Chang’ah, Mkuu wa Wilaya hiyo, amesema kuwa wanafunzi wa kike kupewa mimba wilayani humo limefanywa kama ni utaratibu wa kawaida huku akidai serikali inaanza kuangalia namna ya kuanza kujenga majengo (mabweni) kwenye shule ili kupunguza tatizo hilo.

Chang’ah amesema kuwa Serikali imezungumza na viongozi wote ikiwemo mahakimu kuhakisha kesi zinazohusu mwanafunzi kupewa ujauzito zinaendeshwa na hukumu yake kutolewa mapema ili kutoa fundisho kwa watu wengine wanaoendelea kufanya vitendo hivyo.

Baadhi ya wanafunzi zaidi ya 15 waliopewa ujauzito (majina yanahifadhiwa) waliuambia Mtandao Huu, kwamba sababu zilizochangia kupewa mimba ni kutokana na kurubuniwa kwa kupewa hongo ya fedha na vitu mbalimbali.

Wanafunzi hao ambao wengi wana umri wa kuanzia miaka 16 wakiwa ni wa shule za msingi na sekondari, walipoulizwa ni kiasi gani cha fedha walichokuwa wakipewa, wangine walisema walikuwa wanapewa Sh. 5000 na wengine Sh. 20, 000.

Jiachim Joasen, Mmoja wa kijana aliyempa mimba mwanafunzi,  alisema kuwa alikutana na mpenzi wake ambaye kwa sasa wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miezi miwili, mwaka 2015 akiwa nyumbani kwao baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka shule.

Joasen amesema kuwa yeye alikutana na mwanafunzi huyo akiwa nyumbani na kwamba Machi 2016 Oparesheni ya kukamata wazazi ambao hajapeleka watoto shule ilipoanza ndipo wazazi wake walimpeleka shule huku akidai hawakuacha mapenzi yao.

Katika msako uliofanyika juzi kwenye zaidi ya kata sita, umefanikiwa kuwakamata wazazi 9, wanafunzi 16 na kijana mmoja ambaye alimpa ujauzito mwanafunzi huku vijana wengine wakikimbia baada ya kusikia msako huo ukiendeshwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!