Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wampuuza Makonda: Tujiandikishe ili iweje?
Habari za SiasaTangulizi

Wampuuza Makonda: Tujiandikishe ili iweje?

Spread the love

BAADHI ya wafanyabiashara wamepuuza agizo la Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam la kufungua maduka yao kuanzia saa tano asubuhi leo tarehe 14 Oktoba 2019. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Wameeleza kuwa, hawana sababu za kujiandikisha kwa kuwa nchi imezama katika siasa za upande mmoja, huku vyama vya upinzani vikiminywa.

Gasper Shirima, ni miongoni mwa wananchi jijini Dar es Salaam wanaoeleza sababu za kutojiandikisha pia kukerwa na kile alichokiita ‘siasa za upande mmoja.’

“Sijajiandikisha, siasa zenyewe zinaonekana za upande mmoja. Kwa nini tupate shida ya kujiandikisha? Kuna haja gani ya kupoteza muda?

“Kama watu wamenyimwa haki ya kufanya shughuli za chama, kujiandikisha mapema kuna haja gani sasa? wakati wenzetu wameshajiandaa siku nyingi kujenga vyama, hakuna sababu,” amesema Shirima.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam jana tarehe 13 Oktoba 2019, iliwataka wafanyabiashara jijini humo kuchelewa kufungua biashara zao leo ili kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki uandikishaji kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019.

Shaban Yusuph, Mfanyabaishara wa Sinza-Uzuri amesema, hajatekeleza agizo hilo, kwa kile alichoeleza kwamba ni la ‘uzinguaji.’

“Ah! anazingua huyo,” amesema Yusuph na alipoulizwa kama tayari amejiandikisha, amesema “umeniuliza kama nimejiandikisha, nikikwambia ndio au hapana utajuaje?”

Robert Duvi, Mfanyabaishara wa Kinondoni alipohojiwa sababu za kufungua duka lake kabla ya muda ili kutekeleza agizo la Makonda, amejibu, hatojiandikisha kwa kuwa hana mpango wa kupiga kura.

“Nijiandikishe ili iweje? Sina mpango wa kupiga kura, sitaki kupiga kura,” amesema Duvi.

Cyprian Lonjini, Mfanyabiashara wa Kinondoni ameuambia mtandao huu kwamba, agizo la kuchelewa kufungua maduka hakulisikia.

“Sijalisikia agizo, lakini pia nimejiandikisha, katika kituo cha Mwananyamala,” amesema Lonjini.

Zoezi la uandikishaji wapiga kura lilianza tarehe 8 Oktoba mwaka huu na linatarajia kumalizika siku ya alhamisi tarehe 17 Oktoba mwaka 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!