Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliouwa Watanzania Msumbiji wanaswa, mmoja afariki
Habari Mchanganyiko

Waliouwa Watanzania Msumbiji wanaswa, mmoja afariki

IGP Simon Sirro
Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema, watu watano wanaoshukiwa kuhusika katika tukio la mauaji ya Watanzania tisa nchini Msumbiji, wanashikiliwa na vyombo vya dola nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

IGP Sirro amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa nyumba 20 za polisi mkoani Geita leo tarehe 15 Julai 2019.

Aidha, IGP Sirro amesema mtuhumiwa mmoja kati ya watano waliokamatwa, amefariki dunia.

“Hata tukio la Msumbiji, niliahidi kwa Watanzania kwamba waliofanya hilo tukio, damu ya Watanzania haipotei bure. Mpaka sasa watu watano wamekamatwa na mmoja wao ametangulia mbele ya haki na wanatajana,” amesema IGP Sirro.

Wakati huo huo, IGP Sirro amesema mpango wa utekelezaji wa tukio hilo ulifanyika nchini Tanzania, huku utekelezaji wake ukifanyika nchini Msumbiji.

IGP Sirro amesema, Jeshi la Polisi nchini linashirikiana na Jeshi la Polisi la Msumbiji kuwachukulia hatua waliohusika na mauaji hayo.

“Inaonekana kwa kweli plan ‘mpango’ yote ilifanyika nchini kwetu, tukio lilifanyika Msumbiji. Kimsingi wote wamepatikana wanaendelea kutajana, operesheni inafanyika kwa kushirikiana na wenzetu wa Msumbiji,” amesema IGP Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!