Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waliotafuna fedha za korosho matatani 
Habari za Siasa

Waliotafuna fedha za korosho matatani 

Spread the love

MAMA Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwashughulikie watu waliodhurumu fedha za malipo ya korosho kupitia Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mazao(AMCOS). Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Samia ametoa agizo hilo leo Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 wakati akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika Uwanja wa Polisi Jimbo la Nanyamba mkoani Nanyamba mkoani Mtwara.

Samia ameiagiza Takukuru ihakikishe waliodhurumiwa fedha za korosho walipwe stahiki zao.

“Kulikuwa na deni kubwa la korosho na Serikali tumelipa lote, lakini viongozi wa AMCOS wameangalia nani hajui kusoma pesa zao wakazichukua, naiagiza Serikali ya Mkoa kila aliyedhurumiwa kupitia Takukuru pesa ipatikane,” amesema Samia.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imelipa deni lote la fedha za korosho, hivyo wanaolalamika hawajapata fedha mamlaka husika zinatakiwa zitafute ufumbuzi wa mahali ziliko fedha zao.

“Serikali tumelipa deni lote, lakini viongozi wa ushirika wanafanya mambo yasiyoingilika akilini, Rais Magufuli alishatoa Sh.20 bilioni kwa malipo ya Korosho, zipo Mtwara zitafutwe wapi zimeingia wanaodai walipwe pesa zao,” amesema Samia.

Mgombea huyo wa urais amemaliza mkutano wake wa kwanza kati ya miwili na sasa ameondoka kwenda kuendelea na mkutano mwingine mkoani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!