Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Walionunua magari ya kifahari serikalini matumbo joto
Habari za Siasa

Walionunua magari ya kifahari serikalini matumbo joto

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa siku saba kwa katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, maofisa wanaochambua maombi ya ununuzi wa magari ofisi ya waziri mkuu na wakurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halmashauri ya wilaya ya Chato, Msalala na Kahama wajieleze kwa sababu gani magari hayo yalinunuliwa kwa gharama kubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi, tarehe 17 Desemba  2020, wakati akizungumza na watumishi wa umma, wabunge, madiwani katika jiji la Mwanza na Manispaa za Ilemela na Nyamagana katika hoteli ya Malaika, jijini Mwanza.

Amesema magari hayo ni mzigo kwa wananchi.

Majaliwa amesema hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na haiwezekani viongozi hao watumie magari ya gharama kubwa badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na kutaka muongozo wa ununuzi wa magari uliotolewa na Serikali uzingatiwe.

Amesema, matumizi ya fedha za umma lazima yasimamiwe ipasavyo na kwamba Serikali haina mzaha na mtumishi yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha za umma, hivyo amewataka madiwani wakasimamie vizuri maeneo yao.

Waziri mkuu amewataka wakurugenzi wahakikishe wanatoa ushauri ipasavyo katika mabaraza ya madiwani kuhusu matumizi na manunuzi, pia watoe kipaumbele katika udhibiti wa mapato na rasilimali za umma.

“Wakurugenzi zingatieni vipaumbele vya wananchi na Halmashauri zetu katika kupanga matumizi na manunuzi na tumieni fedha za mapato ya ndani kutekeleza miradi ya kimkakati.”

Waziri Mkuu amewataka viongozi wa halmashauri waweke mikakati madhubuti itakayowezesha makusanyo ya Halmashauri zao yafikie asilimia 100 au zaidi.

“Kuweni wabunifu wa vyanzo vipya vya mapato na ongezeni kasi ya ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri zenu.”

Kadhalika, waziri mkuu amewataka watumishi wa umma wahakikishe wanawafuata wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini walipo na kuwasikiliza kero zao na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Majaliwa amerejea kauli yake aliyoitoa tarehe 7 Desemba  2020 ya kuwataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini wahakikishe kuwa watumishi wa idara nzima ya elimu hawaendi likizo mwisho wa mwaka huu, badala yake wakasimamie ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati na wawe wamekamilisha ifikapo 28 Februari  2021.

“Watumishi wa idara ya Elimu Maafisa Elimu Wilaya na Mkoa, Wahandisi wa ujenzi, Maafisa Manunuzi wa Wilaya na Wakurugenzi wasipewe likizo kipindi hiki kuelekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya hadi 28 Februari, 2020 ili wakamilishe ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 3,000 kwa ajili ya wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza ili waweze kuingia madarasani.”

Kuhusu suala la kufanya ibada siku ya Krismas na Mwaka Mpya, Waziri Mkuu amesema watumishi hao hawajazuiwa kufanya ibada na badala yake watasali vituoni kwao na kwamba hajazuia watumishi hao kufanya ibada wakati wa sikukuu hizo.

Jumatatu, 7 Desemba 2020 Waziri Mkuu aliendesha kikao na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa njia ya video akiwa ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma na kupokea taarifa ya maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!