Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakulima waomba mbegu za muda mfupi
Habari Mchanganyiko

Wakulima waomba mbegu za muda mfupi

mazao la Alizeti
Spread the love

JUKWAA la Wakulima wanawake wilayani Chamwino (JUWWACHA) limeishauri serikali kutilia mkazo matumizi ya mbegu za muda mfupi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wilayani humo. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akisoma mapendekezo ya jukwaa hilo linalowezeshwa na Shirika la Action Aid, Mhasibu wa jukwaa hilo, Nuru Mpanda alisema kutokana na wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye msimu wa kilimo wanashauri mkazo huo utiliwe ili waweze kupata mavuno mengi.

Pamoja na hayo, alisema pia serikali ipanue na kuimarisha mifumo ya umwagiliaji kama ilivyo kwa kata za Buigiri, Chalinze, Fufu, Suli na Chiboli ili kukabiliana na hali hiyo.

“Pia tunapendekeza mashine ya kupima afya ya udongo zinunuliwe na zitumike vijijini kwa ajili ya kuimarisha matumizi sahihi ya mbolea na mbegu,” alisema.

Alieleza kuwa wananchi wengi hawatumii mbolea kwa sababu mbalimbali, ikiwemo matumizi yanayohitaji kujua afya ya udongo ili kujua upungufu wa madini yanayokosekana kwenye udongo.

Alisema uwepo wa mashine hizo na huduma bora za ugani zitasaidia uzalishaji wa mazao wenye tija kwa wakulima.

Aidha alitaka taarifa za hali ya hewa kwa wakulima zitolewe kwa wakati ili wakulima waweze kujua kiwango cha mvua kilichopo kwenye maeneo yao.

Kadhalika, alisema changamoto nyingine zinazowakabili wakulima ni bei ya pembejeo kuwa ghali na kusababisha mkulima mdogo kushindwa kumudu.

Alisema kwa zao la alizeti mbegu ni ghali ambapo zinauzwa kuanzia Sh. 8,000 hadi Sh. 35,000 kwa kilo moja kutegemea na aina ya mbegu.

Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Samweli Kaweya aliwataka wakulima hao kutumia maghala ya ushirikia ili kuepuka janga la kuuza mazao bila sababu za msingi.

Alisema wakulima wengi wamekuwa wakiuza mazao bila utaratibu wa kutohifadhi mazao katika maghala ya kuhifadhia mazao hayo na kusababisha familia nyingi kukosa chakula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!