Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Wakorea kuwapiga tafu TFF kuinua soka la Vijana
Michezo

Wakorea kuwapiga tafu TFF kuinua soka la Vijana

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF$, leo imengia makubariano na Shirika la Maendeleo nchini Korea (KIDC) kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu wa vijana kwa wanawake kwa kuleta wakufunzi katika kipindi cha miaka miwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Katika makubaliano hayo KIDC italeta wataalamu wapatao 30 katika shule zilizopo kwenye mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Fountain gate, Jangwani, Kibasila, Chang’ombe na Benjamini Mkapa katika kipindi cha mwaka mmoja na baadae kuendelea katika mikoa mingine.

Baada ya makubaliano hayo Rais wa TFF Wallace Karia alieleza kuwa wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha malengo kwenye soka la wanawake kwa kuwa bajeti yao ni ndogo ili kufanikisha kucheza kombe la dunia lililo mbele.

“Makubaliano haya tunaingia leo ni ya miaka miwili ambapo KIDC kufikia mwezi Disemba mpaka juni watakuwa wameleta wataalamu 30 kwa ajili ya kuendeleza program hiyo ambapo itaanza katika baadhi ya shule kwenye mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Karia.

Katika hatua nyingine Karia amesema kuwa kwenye mkataba huo pia TFF itafaidika kwa kupata wataalamu watatu ambao wawili watakuwa ndani ya idara ya habari na mmoja kwenye idara ya ufundi katika kipindi cha mwaka mmoja. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!