
Uhuru Kenyatta na Raila Odinga
BAADA ya vuta nikuvute za kampeni kali za uchaguzi mkuu nchini Kenya hatimaye wananchi wa nchi hiyo wanatarajia kupiga kura kumchagua Rais na viongozi wengine wa kisiasa, anaandika Hamisi Mguta.
Kuna wagombea wanane katika uchaguzi huo, lakini wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha rais ni Raila Odinga ambaye anatokana na muungano wa National Super Alliance (NASA) na Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.

Uchaguzi huo utafanyika kesho Agost 8 na kampeni zilifungwa jumamosi ambazo zilionyesha waanasiasa hao wawili wakichuana vikali kupitia mikutano ya hadhara.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema kwamba unapofanyika uchaguzi mkuu nchini humo, kinachohofiwa siyo nani atashinda bali huyo akayeshindwa kama atakubali matokeo.
Viongozi hao wawili walifanya mikutano miwili ya mwisho siku ya Jumamosi ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu.

Odinga alikuwa kwenye bustani za Uhuru Park, mjini Nairobi, huku Kenyatta akiongoza mkutano wake katika uwanja wa Afraha Stadium, Nakuru, takriban kilomita 160 kutoka Nairobi.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe