Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakazi wa Dar wajitokeza kuchangia damu
Habari Mchanganyiko

Wakazi wa Dar wajitokeza kuchangia damu

Spread the love

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali vya kuchangia damu salama, kwa lengo kuongezewa katika benki ya damu Tanzania, anaandika Jasmin Seif.

Zoezi hilo lililofanyika katika vituo vya Damu Salama Mnazi Mmoja, Hospitali ya Muhimbili, Karume, Hospitali ya Amana, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Lugalo na Hospitali ya Sinza Palestina.

Wakazi hao wameonesha kuguswa na tukio hilo kutokana na matukio yaliyowatokea baadhi yao huku wengine wakiwa wameondokewa na ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ukosefu wa damu mahospitalini.

Asha Saidi mkazi wa Buguruni ni miongoni mwa wakazi waliojitokeza kuchangia damu huku wakiwa wameguswa moja kwa moja na athari za ukosefu wa damu mahospitalini.

“Leo nimejitokeza kuja kutoa damu huku nikiwa na uchungu mkubwa sana, kwani mwaka jana nimepoteza mtoto wangu katika hospitali ya Amana kwa kukosa damu,” amesema Asha Said.

Mbali ya watu kuchangia damu, wengine walijitokeza kutoa misaada kwa waliokuwa wanachangia damu kama maji, juisi, matunda na biskuti kwa ajili ya waliojitolea damu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!