Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakandarasi wazawa waililia serikali
Habari Mchanganyiko

Wakandarasi wazawa waililia serikali

Ujenzi reli ya kisasa
Spread the love

VYAMA vya wakandarasi vya Contractors Association of Tanzania, Tanzania Civic Engineering Contractors na Association of Citizen Contractors, wameiomba serikali iendelee kutoa fursa za kazi kwenye ujenzi wa miundombinu nchini, anaandika Angel Willium.

Wakandarasi hao wameiomba serikali kupata kazi ya kujenga miundombinu kama reli, nishati, bomba la kusafirisha mafuta, ujenzi wa Makao Makuu ya Dodoma na sekta ya maji kwa wakandarasi wazawa.

Mwenyekiti wa Vyama vya Wakandarasi, Injinia Lawrence Mwakyambiki amesema hayo wakati akitambulisha siku ya wakandarasi ambayo itakayofanyika kila mwaka, kuwa wakipewa kazi hizo pesa watakazopata zitatumika kuinua uchumi ndani ya nchi.

“Wakandarasi wa hapa nchini wanaweza kukuza uchumi wa kwa sababu pesa wanazopata katika ujenzi zitasaidia kujenga hoteli au shule nchini kwetu,’’ amesema Injinia Mwakyambiki.

Injinia Mwakyambiki amesema lengo ya kuwa na siku ya wakandarasi ni kubadilishana uzoefu katika utendaji wa miradi mbalimbali na kutoa fursa kwa washiriki 200-300.

Aidha Injinia Mwakyambili amesema wanawashukuru wadau wa wakandarasi wakiwemo Commercial Bank of Afrika (CBA) na NMB Bank na wafadhili wengine kwa kuendelae kufanya kazi na wakandarasi wazawa.

Siku ya wakandarasi imepangwa kufanyika Novemba 17, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Das es Salaam na itakuwa ikifanyika tarehe hiyo kila mwaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!