Waislamu washauriwa kusaidia wenye mahitaji – MwanaHALISI Online
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu

Waislamu washauriwa kusaidia wenye mahitaji

WAUNINI wa dini ya Kiislamu nchini wametakiwa kuisaidia jamii yenye uhitaji bila kujali itikadi za kidini, ananadika Dany Tibason.

Hayo yamebainishwa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu muda mfupi baada ya kumalizika ibada ya katika msikiti wa Gadaffi mjini hapa.

Kiongozi huyo wa kiroho amsema ili kufikisha mapenzi ya kiongozi mkuu wa dini hiyo ni lazima ukajua jinsi ya kumtumikia Mungu kwa njia ya utoaji ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wenye uhitaji.

Akizungumzia wale wanaokwenda kuhiji amesema wanapokwenda Hija watambue kuwa wanaenda kufanya ibada takatifu na ili kutimiza ibada hiyo ni lazima wanapoondoka wakaacha hakuna malalamiko wala manung’uniko ya aina yoyote.

“Wale wote wanaoenda Hija ni lazima wakatambua kuwa wanakwenda katika ibada muhimu kweli kweli na ili kuweza kutimiza malengo ni jambo la msingi sana kuziacha familia au majirani wakiwa na furaha na hakuna malalamiko ya aina yoyote” amesema Sheikh Rajabu.

Aidha, ametoa wito kwa waumini wote wa dini hiyo kuhakikisha wanafanya maombi ya kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali ili amani na uchumi viwepo na iwe faraja kwa Watanzania.

WAUNINI wa dini ya Kiislamu nchini wametakiwa kuisaidia jamii yenye uhitaji bila kujali itikadi za kidini, ananadika Dany Tibason. Hayo yamebainishwa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu muda mfupi baada ya kumalizika ibada ya katika msikiti wa Gadaffi mjini hapa. Kiongozi huyo wa kiroho amsema ili kufikisha mapenzi ya kiongozi mkuu wa dini hiyo ni lazima ukajua jinsi ya kumtumikia Mungu kwa njia ya utoaji ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wenye uhitaji. Akizungumzia wale wanaokwenda kuhiji amesema wanapokwenda Hija watambue kuwa wanaenda kufanya ibada takatifu na ili kutimiza ibada hiyo ni lazima wanapoondoka wakaacha hakuna malalamiko wala manung’uniko…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Dany Tibason

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube