Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wagonjwa wa corona wafikia 2,474 Kenya, Rais Uhuru asubiriwa
Kimataifa

Wagonjwa wa corona wafikia 2,474 Kenya, Rais Uhuru asubiriwa

Spread the love

SERIKALI ya Kenya imesema, wagonjwa wa corona (COVID-19) nchini huyo wamefikia 2,474. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, Katibu wa Wizara ya Afya wa Kenya, Dk. Mercy Mwangangi alisema idadi hiyo imefikiwa baada ya wagonjwa wapya 134 kukutwa na corona.

Alisema wagonjwa hao wapya 134 ni matokeo ya vipimo vilivyofanywa kwa watu 3,177.

Dk. Mwangangi alisema, kati ya hao 134, watatu ni raia wan je na 131 ni Wakenya. 98 ni wanaume na 36 wanawake.

Alisema hadi jana, watu waliokuwa wamepimwa virusi vya corona walikuwa 90,875.

Dk. Mwangangi alisema, wagonjwa hao 134 wapo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ambao ni; Mombasa (67), Nairobi (31), Busia (15), Machakos (5), Taita Taveta (4), Kilifi (2), Nakuru (2), Garissa (1), Murang’a (1), Kisumu (1), Uasin Gishu (1) and Kajiado (1).

Alisema, wagonjwa 51 waliopona corona wameruhusiwa kutoka hospitalini hivyo kufikishwa idadi ya wagonjwa 643 waliopa mpaka jana Ijumaa.

Mtandao wa Worldometer, hadi leo Jumamosi tarehe 6 Juni 2020, umeripoti wagonjwa 3,362,308waliopona duniani, vifo vikiwa 398,535 huku maambukizo yakiwa 6,866,120

Kenya, inasubiri kupata mwelekeo mpya wa jinsi wa kuishi katikati ya janga la corona baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuhutubia Taifa hilo leo Jumamosi.

Wakenya wanasubiri kuona, endapo Rais Uhuru ataregeza masharti ili kuruhusu wananchi kufanya shughuli zao kama kawaida na kupunguza ugumu wa maisha ikiwemo kutoa nafuu ya masuala ya kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!