Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli atapata lini ‘First Eleven’ ya serikali yake?
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli atapata lini ‘First Eleven’ ya serikali yake?

Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli, amemng’oa kwenye wadhifa wake, Kamishena Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere na kumteuwa Edwin Mhende, kushika nafasi yake. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Kichere anakuwa Kamishena wa tano wa TRA kung’olewa katika nafasi hiyo, tangu Rais Magufuli kushika madaraka ya urais, Novemba mwaka 2015.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais (Ikulu), leo tarehe 8 Juni 2019 na kusainiwa na mkurugenzi wake, Gerson Msigwa, haikueleza sababu ya kung’olewa kwa Kichere.

Hata hivyo, kuondolewa kwa Kichere kwenye nafasi ya Kamishena Mkuu wa TRA, kumekuja siku moja tangu Rais Magufuli, amalize kukutana na wafanyabiashara mbalimbali, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Aliyekuwa wa kwanza kuonja pangua pangua ya Magufuli pale TRA, alikuwa Rished Bade, ambaye aliteuliwa kuwa Kamishena Mkuu wa mamlaka hiyo na Rais Jakaya Kikwete, tarehe 6 Mei 2014. Bade aling’olewa kwenye nafasi yake, mwezi wa kwanza wa Rais Magufuli, kuwa Ikulu –tarehe 27 Novemba 2015. 

Bade alirithiwa na Dk. Phillip Mpango, ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo Novemba 2015 na kuondoka tarehe 23 Desemba 2015.

Kwa sasa, Dk. Mpango, ni waziri wa fedha na mipango. Haijulikani kama Dk. Mpango, naye iwapo naye atamaliza ubunge wake akiwa bado waziri wa fedha na mipango.

Nafasi ya Dk. Mpango ilirithiwa na Eliakimu Maswi, aliyefanywa kuwa Kaimu Naibu Kamishena Mkuu wa TRA, 30 Desemba 2015 na kuondoka Januari 2016. 

Baada ya Maswi “kutumbuliwa,” Rais Magufuli alimteua Alphayo Kidata, kuwa Kamishena mkuu wa mamlaka hiyo ya mapato. Kidata alihudumu katika wadhifa huo, kuanzia Januari 2016 hadi 25 Machi 2017 alipoondolewa na kufanywa kuwa katibu mkuu (Ikulu). 

Kidata, alirithiwa na Kichere ambaye ameong’olewa mara baada ya kumalizika mkutano wa jana kati ya rais na wafanyabiashara.

Katika mkutano wa jana, rais alipokea malalamiko lukuki kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara aliokutana nao, huku wengi wao wakiituhumu TRA, kwa walichokiita, “utendaji mbovu.”

Akizungumza katika mkutano huo, mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma, mbali na kumtaka Rais Magufuli, kumuondoa waziri wa viwanda na biashara, JosephKakunda, aliituhumu TRA kuwa chanzo cha kuzorota kwa biashara nchini.

Naye Hussein Nassor, aliyejitambulisha kama mfanyabiashara kutoka mkoa wa Geita, aliutumia mkutano huo kuituhumu TRA kwa uongozi mbovu; na kumtaka rais kuufumua uongozi uliopo sasa kwa maelezo kuwa unakandamiza wafanyabiashara.

Alisema, “TRA inafanya kazi vizuri, lakini kuna baadhi ya wafanyakazi wake sio waaminifu. Kuna fedha za serikali zinapotea, tena nyingi mno. Naamini usiri huu utakapoondoka serikali itakusanya fedha nyingi.”

Alisema, “kwa mfano, kontena moja unaweza ukaambiwa huyu ametoa kodi ya Sh. 10 milioni, huyu Sh. 20 milioni na huyu Sh. 30 milioni. Na huu ukwepaji hautaisha, ni vema TRA ikafumuliwa kidogo, baadhi ya sheria zibadilishwe ili pawe na uwazi.”

Alisema, “wafanyabaishara wengi nchini wamepalalaizi kimawazo na kibiashara,” kutokana na kusumbuliwa na na mamlaka hiyo ya mapato na kuongeza, kwa maoni yake, iwapo itaweza kufumuliwa, angalau inaweza kuleta tija huko mbele.

Kuhusu Kakunda, akionekana kama ametumwa, mbunge Msukuma alisema, “hakuna mfanyabiashara yeyote kati ya waliyopo hapa, anayemfahamu waziri wa viwanda na biashara. Kila kitu ni waziri wa fedha.”

Alisema, “mimi nakushauri, huyu bwana ameshindwa kazi. Vunja wizara hii na kuinganisha na wizara ya fedha na utaona matunda yake.” 

Rais ametengua pia uteuzi wa Kakunda. Amemkabidhi nafasi hiyo, Innocent Bashungwa, aliyekuwa naibu waziri wa kilimo.

Kung’olewa kwa Kakunda, aliyechukua mikoba ya uongozi kutoka kwa Charles Mwijage, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa tarehe 10 Novemba 2018. 

Kakunda amedumu katika nafasi hiyo kwa siku 210.

Katika mabadiliko hayo, Kamishena Kichere amefanywa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe. Amechukua nafasi ya Erick Shitindi, ambaye amestaafu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!